Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

JF. Where we dare to talk openly.

Kuna watu ni jasiri kuandika wanachoandika wakiwa hapa JF pekee, huku wakitumia majina bandia . Wakiwa kwenye ulimwengu halisi....... inakuwa tofauti kabisa. Haya ndiyo maisha. Kazi inaendeleaa.
Hapo si ajabu mtoa mada katoka kula ugali wa kulumangia na dagaa mchele, sasa hivi yuko zake kitandani mkonononi na smatfon yake iliyopasuka kioo huku mkono mwingine ukifanya kazi ya kufukuza mbu
 
Dar es salaam ni taaabu sana.
 
Upo sahihi kabisa. Sababu ni serikali yako. Usafiri umefanywa kuwa anasa badala ya hitaji muhimu la watu.

Nchi zilizoendelea magari ni hitaji la muhimu
 
Kutumia tecno au infinix ni umaskin kivip?dogo acha ulimbuken wenye pesa wanatumia simza kawaida tu ila maskn ndo mbwembwe kibao
 
Sijawahi kufuatilia kujua rank ya umaskini kwa Tanzania unaanzia mtu awe/apate bei gani kwa siku au amiliki nini ili kumtofautisha na wale hohehae!

Mf;wapo watu a'cally kutokana na mazingira waliyoishi/kulia yaliwafanya kuwa tu social,uwezo wa kuhudumia gari wanao even kumiliki hizi baby walker zaidi ya moja wanao ila haiingii akilini eti mtu ujibane ili ununue gari kwa kuogopa kupanda daladala,maisha ni yako ninyi mnaoona aibu kupanda daladala mnaogopa macho ya watu hamjui kwamba mumiliki gari au musimiliki gari hamuwapunguzii wala kuwaongezea chochote wale mnaohisi wanawatazama.

Mimi nina Bajaj tatu mpya zinazunguka barabarani ila ukinikuta kwenye Mwendokasi kama siyo mimi vile yote ni kwa sababu naishi maisha yangu Tanzania hii ukiogopa ogopa vitu vidogo vidogo kama kupanda public buses kuna baadhi ya vitu vitaku-cost.
 
Kaka umaskini mbaya sanaaa,pata hata kisent usahau hyo kitu.Nawashangaa watu wanaoonaga kua nyumba ni ya kwanza Kabla ya kagari ka millioni8
 
Ni utoto tu ukikua utaacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…