Kwa kuwa umesema, huyo dada sio mtu wa kukwapua wanaume za watu, na kwa mumeo imetokea kibahati mbaya na hajui km baba ni mume wa mtu.
Basi muitee huyo dada na umpe onyoo kalii, naamini atamuacha chibaba wako.
Hiyo njia unayotaka kutumia, uta fail na uta fail haswaa, niamini mie.
Usijesema hukuambiwaa. Poleeeee sanaa.
Mmenikumbisha zamani, enzi niko na hekaheka za mahaba eehehehehe....
Nilifanya huu umafia, hivyo namuelewa mtoa mada na kwangu ilifanya kazi asilimia elfu na nilipata mrejesho.
Kwangu ilikuwa hivi....
Niko zangu nimetulia kigori naendesha maisha yangu, akaja jamaa tabasamu la Kasinde na sauti vikamzingua, akaniimbisha weeeh hadi nikaingia boksi. Kosa langu kabla sijamfahamu vya kutosha wasifu, wandani na hulka yake nikazama mazima.... hatukufunga ndoa nilachomoka ila chamoto nilikiona....
Siku ya kwanza namvulia chupi, japo nilimuweka kona tupime VVU kwa mbinde sana alikubali, nakumbuka tulienda agakhan eehehehee huu ulikuwa mtihani wangu mkubwa maana najua ndomu itaacha kutumika baada ya mwezi tuu sasa hapo kama hujajua afya yake unaanza kufa kihoro. Mweeh wacha nifupishe kidogo maana najikuta naelezea bwereree akati hapa nachangia mada tuu...
Siku ya kwanza ya chezo jamaa hakufanya kosa, alinipa maufundi nikabwaga moyo na akili, alipoona ashaniweka mateka wake sichomoki, nikaanza ona makucha yake, sms za wanawake kibao huyu mmoja nikabanana nae achague huyo mwanamke au mimi. Akajitetea ooh hatujagombana siwezi muacha na yeye ndo alitangulia kuwa nae kwenye mahusiano, mimi nilikuja tongozwa baadae....eehehehe....
Nikaona huyu ananichezea, kuniacha hataki kumuacha huyo mwanamke wake hataki, nikamfata kijana mmoja (mchaga) alikuwa ndo ametoka kuachana na gelofrendi wake, nikampatia namba ya simu, picha, anakoishi, anakofanya kazi, na wasifu wa dada. Huyo dada alikuwa binti wa kutoka Kigoma, alikuwa mrembo kweli nahisi alichanganya na unyarwanda akati Kasinde hapa no tako no wati, tabasamu tuu...🙄🙄
Ilifanya kazi huyo dada akakolea kwa huyu kijana wa kichaga akamuacha jamaa wangu nikabaki nakula mtulinga pekeyangu. Hivyo mbinu anayotaka kuitumia mtoa mada kwangu ilifanya kazi ila sasa.... jasiri haachi asili.... ni kweli yule dada waliachana ila ilifungua milango kwa wanawake wengine... ni mwanaume ambae hawezi kaa na uhusiano wa wanawake 2 au 3... yeye ni bunch of ladies.....😱😱😱
Yakanishinda nikabwaga manyanga.
Kila la kheri mtoa mada.
Kasinde Mahaba Matata 😉.