Mi wazee nawaheshimu sana.
Kuna Bar Moja nilienda hapo tabata Aroma, kuangalia mishe ya umeneja wa Bar.
nikamkuta mzee mmoja anagonga konyagi yani yuko tungi aisee mida ya saa nne asubuhi..
Mzee yule nimemkuta meza za mwanzo kabisa nikamsalimia vizuri akaitika. Nikaenda counter nikawaambia nimeleta CV zangu kwa kazi flani.
Wakanipokea, nikakaa pale kama nusu saa nasubiri INTERVIEW.
Baada ya muda yule dada wa counter akaniita ananiambia mzee anakuita (yule niliemsalimia mwanzoni) kwa ajili ya interview.
Dah nilijiuliza maswali mengi sana endapo ningempita bila salam ingekuwaje.
mzee tukasalimiana tena akaniomba vyeti na barua, akatazama pale huku anasifia.
Hapo hapo akaniambia You are my new Bar manager[emoji3062][emoji3062][emoji28][emoji28][emoji28]
Jamani nilifurahi sana! nimekula laki 3 tatu hapo na posho miezi mitano nashukuru mpaka sasa nina mtaji wa Biashara