Binafsi huwa nawapisha siti, ila mostly inategemeana maana Ni tendo la kiutu na siyo lazima.
Kuna siku nilikuwa natoka Bukoba kuja Mwanza, nikawa nimepanda stand Bukoba kwahiyo nikapata siti.
Bus lilipofika Muleba akapanda Mzee mmoja, ila alikuta siti zimeisha baada ya KUSIMAMA kwa muda mrefu, akaniomba, kijana naomba nikupe 1,000 (elfu moja) nikae.
Nilivyomuona nikaona kweli anahitaji kukaa Wala buku lake sihitaji. Nikamwambia kaa tu mzee Wala usijali.
Tulivyofika Busisi Ferry akanitafuta, anilipie Ferry nikwamwambia Haina haha mzee.
Sometimes, hivi Ni viti ambavyo hata havikuumizi ukivifanya. Kwahiyo sioni shida.
Tatizo kubwa na baadhi ya wazee kwa Dar kukosa ustaarabu. Yaani unapanda daladala, unapata siti, anakuja mzee unampisha unasimama.
Sasa kumbe mzee mwenyewe anashuka karibu tu, badala akwambie urudi kwenye siti yake yeye anshuka tu anasepa bila hata shukrani utafikiri nlikuwa Ni haki yake.
Na akishuka, kwenye siti anakaa mchizi boti tu , halafu wewe unaendeleaje kushika bomba mpaka mwisho wa Safari.
Huo ndio upuuzi mtupu.