Kaveli
JF-Expert Member
- Dec 4, 2012
- 5,443
- 8,903
- Thread starter
- #41
Ahsante -Kavel-
Kwa Mtazamo wangu na kwa jinsi nilivyouelewa wimbo Huu"shujaa"
Nauweka katika vipande viwili au magagara mawili.
1. Kutokana na wimbi kubwa kwa Sasa la wasanii wa hip hop kumbwelambwela na kushindwa kusimama katika utamaduni wa hip hop..Mfano uimbaji wao na maudhui ya nyimbo.
Hivyo inanifanya kuukumbuka wimbo wake wa "Soko na pesa"
Baada ya kukaa kimya kwa kipindi flani Naweza kusema Shujaa inamuelezea yeye kwa namna moja kwani ni mtu asiyeyumbishwa katika ut amaduni wa hiphop na hawezi kuyumba kamwe.
2.katika upande wa pili hapa kazungumuzia masuala ya utawala/uongozi katika Taifa letu...hapa kidogo pana utata kumutambua Shujaa lakini pia inaweza kuwa kinyume cha shujaa katika upande huu.
"Ukisema milo mitatu utaulizwa Ndio kitu gani"
Nakupenda hip hop zaidi ya machizi wa Mtaa!
Daaah, mkuu nimependa uchambuzi wako. Hasa hiyo para 1, umeonesha ukomavu wako kwenye muziki wetu huu.
Ngoja tuendelee kuichambua hii ngoma. Ina majibu zaidi ya moja, na ina majawabu zaidi ya moja. That's Hip Hop I like.
''Nakupenda sana hipHop zaidi ya machizi wangu wa kitaa, acha wale naokesha nao baa''.
-Kaveli-