Nash Emcee anatualika tumpokee 'shujaa'. Ni shujaa gani huyo?

Ahsante -Kavel-

Kwa Mtazamo wangu na kwa jinsi nilivyouelewa wimbo Huu"shujaa"

Nauweka katika vipande viwili au magagara mawili.
1. Kutokana na wimbi kubwa kwa Sasa la wasanii wa hip hop kumbwelambwela na kushindwa kusimama katika utamaduni wa hip hop..Mfano uimbaji wao na maudhui ya nyimbo.
Hivyo inanifanya kuukumbuka wimbo wake wa "Soko na pesa"

Baada ya kukaa kimya kwa kipindi flani Naweza kusema Shujaa inamuelezea yeye kwa namna moja kwani ni mtu asiyeyumbishwa katika ut amaduni wa hiphop na hawezi kuyumba kamwe.

2.katika upande wa pili hapa kazungumuzia masuala ya utawala/uongozi katika Taifa letu...hapa kidogo pana utata kumutambua Shujaa lakini pia inaweza kuwa kinyume cha shujaa katika upande huu.

"Ukisema milo mitatu utaulizwa Ndio kitu gani"

Nakupenda hip hop zaidi ya machizi wa Mtaa!

Daaah, mkuu nimependa uchambuzi wako. Hasa hiyo para 1, umeonesha ukomavu wako kwenye muziki wetu huu.

Ngoja tuendelee kuichambua hii ngoma. Ina majibu zaidi ya moja, na ina majawabu zaidi ya moja. That's Hip Hop I like.

''Nakupenda sana hipHop zaidi ya machizi wangu wa kitaa, acha wale naokesha nao baa''.

-Kaveli-
 
Mpaka dakika hii, wachangiaji asilimia 98% hawajaung'amua wimbo huu.

SHUJAA huyo ni nani?

-Kaveli-
 
''... watu wamechoka maisha ni taabani mawazo kichwani,
nalia ukame nyumbani, ukisema milo mitatu utaulizwa Ndio kitu gani?" Maalim Nash

-Kaveli-
 
Ni emcee ambaye kama angepewa 'air time' ya kutosha, angekuwa mbali sana. Media industry inawabania sana wanaKilinge. Lakini kimtaa mtaa hawa ndo madoni kwenye game.

-Kaveli-
Kabisa.Kuna mtu anaitwa Sir Lu na wengine kibao wenye uwezo.
 
shujaa anajiongelea yeye mwenyewe.

katika hip hop maalim huwa anajitahidi sana kusimama katika misingi ya hip hop.

nakumbuka kilingeni aliwahi kuwachana kina nick kuacha kutaka kuchana tu badala ya kupata muda wa kutosha kujifunza ,ko nadhan baada ya kupumzika kidogo kutoa ngoma ndo kamua kurudi na kajiita shujaa maana hip hop inaharibiwa na mwack wachache .

cc male
 
Shujaa ni Nash mwenyewe.

Wewe ni mdau wa pili kung'amu hivyo... kwamba huyo SHUJAA ni Nash mwenyewe.

Ila kuna wadau wengi wanang'amua kuwa SHUJAA huyo ni kama mwanasiasa fulani hivi.

Mkuu tuendelee kuisikiliza. Napenda Hip Hop ya aina hii.

-Kaveli-
 
OOh yeaaah. Huyo ndo Nash the real emcee a.k.a galacha wa mitihani. Anasema anaendelea kuandika kuhusu ushenzi alofanyiwa na Tabia.

-Kaveli-
Hahahahah nakubali sana akileta muendelezo wa vitimbi vya kigoli tabia itakua mukide sana.araf ni kweli jamaa mzaliwa wa chigugu masasi?
 
Daaah, mkuu nimependa uchambuzi wako. Hasa hiyo para 1, umeonesha ukomavu wako kwenye muziki wetu huu.

Ngoja tuendelee kuichambua hii ngoma. Ina majibu zaidi ya moja, na ina majawabu zaidi ya moja. That's Hip Hop I like.

''Nakupenda sana hipHop zaidi ya machizi wangu wa kitaa, acha wale naokesha nao baa''.

-Kaveli-
Poa-Mkuu
Tusubiri maoni ya wadau wengine wa hip hop.

"Huu ni muziki wanaharakati unaotetea haki zetu pia,watoto na wenye matiti pia"
 
''...Shujaa tunakuamini sauti ya wanyonge ni wewe,
Paza sauti yako walaUchumi wakuelewe, silaha upewe,
Tetea kwenye elimu kwani Uozo ndo kibao, wanatutia Ujinga wasome watoto wao, ''

SHUJAA huyo ni nani ?

-Kaveli-
 
Hatareee mkuu. Huyo ndo Nash emcee bhana. Daily 'anaandika' ... anaandika kuhusu mambo mengi, na anasema sasa yupo jikoni anaandika kuhusu Babu Seya coz hawakufanya fair.

-Kaveli-
 
Binafsi nang'amua kuwa SHUJAA huyo ni HIP HOP music.

1. ''Hakuna alotegemea kama ungeleja, hasa kipindi hichi ambacho mengi yametokea,
Achana na maneno wapumbavu wanayoongea, kwa vita ulopigana tulidhani ungedondoka,
Kwa ushindi wako huu nakuongezea nyota, kweli umedhihirisha we ni mzizi usiong'oka...''

Hapo Nash anajaribu kuelezea jinsi gani HIP HOP ilivyopitia suppress nyingi na mikwamo ya hapa na pale, mfano media kuibania air time, harakati kadhaa (anti-virus, OKOA hipHop, SUA, n.k) kusinzia na kusuasua, lakini still HIP-HOP imeibuka inaendelea kuwepo. Mikwamo mingi sana hadi wadau hawakutegemea kama hip hop ingeendelea kuwepo.

Pia Maalim anaitia moyo Hip Hop kwamba isijali maneno ya wapinzani na wanaobeza (mfano Hip Hop haiuzi by Madee). Kwa changamoto hizo zote ilivyozivuka na kuendelea kuwepo, basi hip hop imedhihirisha jinsi gani ipo imara and will always be there (KRS ONE kwenye moja ya nyimbo zake aliwahi kusema ''HIP HOP will be there forever, ever''). So maalim anazidi kuupa heshima mziki wa hip hop.

2. ''...Shujaa tunakuamini sauti ya wanyonge ni wewe,
Paza sauti yako walaUchumi wakuelewe, silaha upewe,
Tetea kwenye elimu kwani Uozo ndo kibao, wanatutia Ujinga wasome watoto wao, ''

Hapa maalim anaonesha imani yake kwa Hip Hop kuwa mziki huu ndo sauti pekee ya wanyonge (voice of the voiceless), kwamba ndo mziki pekee wenye kuzungumzia maisha ya mtaa, mziki wenye kuibua yasiyozungumzwa kwenye maisha ya watu wa hali ya chini. (hapa Nash kanikumbusha sana maudhui ya nyimbo moja hivi inaitwa 'On my Block' by 2pac, anaelezea maisha A to Z ya jamii yake kupitia mic).

Nash anaikumbusha hip hop iendelee kuyasemea mambo ya ufisadi na wizi wa viongozi wetu ( wala uchumi). Hali kadhalika maalim anaiambia hip hop itetee na kuanika madudu yaliyopo kwenye elimu yetu ya bongo maana sekta hii imejaa uozo (wizi wa mitihani, kufoji vyeti, n.k).

N.B: SHUJAA = HIP HOP = NASH.

CC Keyon

-Kaveli-
 
Ngoja nimuite na mkuu wangu Lizarazu aje kutusaidia kung'amua pini hii. Ni shujaa gani huyo?

-Kaveli-
"Hakuna aliyetegemea kama ungerejea hasa kipindi hiki ambacho mengi yametokea, achana na maneno wapumbavu wanayoongea, kwa vita uliyopigana tulidhani ungendondoka kwa ushindi wako huu nakuongezea nyota, kweli umedhiirisha wewe ni mzizi usiyong'oka"

Mkuu Kaveli big up sana kwa kuleta hili goma la kusumbua ubongo... Maalim mcee mzee wa V.V.U kwa hii ngoma namfananisha na Hopsin. Ngoma za huyu muhuni huwa zina multiple interpretations.

Kwenye hii ngoma shujaa ni kama thamani "x" kwenye Quadratic equation hapa utapata jibu la positive na negative na yote ni majibu sahihi.

Binafsi hii ngoma naona maudhui yaliyomo yamelenga serikali ya awamu ya tano kwa kiasi kikubwa.

Ukisikiliza mwanzoni mwa verse ya pili(kipande nilichonukuu hapo juu) utaona ni kama ana sifia wapambanaji wa vita vya madawa ya kulevya na kuwapondea wote wanatoa tuhuma dhidi ya bashite. Hapa shujaa ni bashite

Hapo hapo kwenye verse ya pili inaonyesha awamu hii hatuna mtetezi na mtetezi wetu pekee ni kupaza sauti lakini sauti hiyo nani wa kuipaza kila mtu anaogopa!? Hapa inaamisha hatujapata shujaa bado na sisi wenyewe ndio mashujaa lakini hatujui kama sisi ndio mashujaa.

Ngoja ntaendelea baadae...
 
Ngoma kama hizi ndio zinafanya hip hop isiwe na mashabiki wengi... Na nyimbo za akina darasa ziendelee kuwa popular
 
Binafsi nang'amua kuwa SHUJAA huyo ni HIP HOP music.

1. ''Hakuna alotegemea kama ungeleja, hasa kipindi hichi ambacho mengi yametokea,
Achana na maneno wapumbavu wanayoongea, kwa vita ulopigana tulidhani ungedondoka,
Kwa ushindi wako huu nakuongezea nyota, kweli umedhihirisha we ni mzizi usiong'oka...''

Hapo Nash anajaribu kuelezea jinsi gani HIP HOP ilivyopitia suppress nyingi na mikwamo ya hapa na pale, mfano media kuibania air time, harakati kadhaa (anti-virus, OKOA hipHop, SUA, n.k) kusinzia na kusuasua, lakini still HIP-HOP imeibuka inaendelea kuwepo. Mikwamo mingi sana hadi wadau hawakutegemea kama hip hop ingeendelea kuwepo.

Pia Maalim anaitia moyo Hip Hop kwamba isijali maneno ya wapinzani na wanaobeza (mfano Hip Hop haiuzi by Madee). Kwa changamoto hizo zote ilivyozivuka na kuendelea kuwepo, basi hip hop imedhihirisha jinsi gani ipo imara and will always be there (KRS ONE kwenye moja ya nyimbo zake aliwahi kusema ''HIP HOP will be there forever, ever''). So maalim anazidi kuupa heshima mziki wa hip hop.

2. ''...Shujaa tunakuamini sauti ya wanyonge ni wewe,
Paza sauti yako walaUchumi wakuelewe, silaha upewe,
Tetea kwenye elimu kwani Uozo ndo kibao, wanatutia Ujinga wasome watoto wao, ''

Hapa maalim anaonesha imani yake kwa Hip Hop kuwa mziki huu ndo sauti pekee ya wanyonge (voice of the voiceless), kwamba ndo mziki pekee wenye kuzungumzia maisha ya mtaa, mziki wenye kuibua yasiyozungumzwa kwenye maisha ya watu wa hali ya chini. (hapa Nash kanikumbusha sana maudhui ya nyimbo moja hivi inaitwa 'On my Block' by 2pac, anaelezea maisha A to Z ya jamii yake kupitia mic).

Nash anaikumbusha hip hop iendelee kuyasemea mambo ya ufisadi na wizi wa viongozi wetu ( wala uchumi). Hali kadhalika maalim anaiambia hip hop itetee na kuanika madudu yaliyopo kwenye elimu yetu ya bongo maana sekta hii imejaa uozo (wizi wa mitihani, kufoji vyeti, n.k).

N.B: SHUJAA = HIP HOP = NASH.

CC Keyon

-Kaveli-

Mkuu salute kwako umewaza sana arifu.

Maalumu hii ngoma amekusanya matukio mengi sana na kuyaweka humo ndani na kila moja kalipa uzito sawa na ndio maana ina consume a lot of brainpower kung'amua na hatimae kupata kitu kimoja kinacho summerize ngoma nzima.

Ukisikiliza verse ya kwanza na ya pili utaona bora ya pili ndio inayotoa muongozo kwa urahisi na kukupa the whole idea ya ngoma.

Huu muziki wa hip hop bhana muda mwingine ukisimamia misingi yake kwa uthabiti unaleta shida kwa hadhira.

Ndio maana akina joh makini wameamua kukimbilia kutunga nyimbo za disco tu.
 
Binafsi nang'amua kuwa SHUJAA huyo ni HIP HOP music.

1. ''Hakuna alotegemea kama ungeleja, hasa kipindi hichi ambacho mengi yametokea,
Achana na maneno wapumbavu wanayoongea, kwa vita ulopigana tulidhani ungedondoka,
Kwa ushindi wako huu nakuongezea nyota, kweli umedhihirisha we ni mzizi usiong'oka...''

Hapo Nash anajaribu kuelezea jinsi gani HIP HOP ilivyopitia suppress nyingi na mikwamo ya hapa na pale, mfano media kuibania air time, harakati kadhaa (anti-virus, OKOA hipHop, SUA, n.k) kusinzia na kusuasua, lakini still HIP-HOP imeibuka inaendelea kuwepo. Mikwamo mingi sana hadi wadau hawakutegemea kama hip hop ingeendelea kuwepo.

Pia Maalim anaitia moyo Hip Hop kwamba isijali maneno ya wapinzani na wanaobeza (mfano Hip Hop haiuzi by Madee). Kwa changamoto hizo zote ilivyozivuka na kuendelea kuwepo, basi hip hop imedhihirisha jinsi gani ipo imara and will always be there (KRS ONE kwenye moja ya nyimbo zake aliwahi kusema ''HIP HOP will be there forever, ever''). So maalim anazidi kuupa heshima mziki wa hip hop.

2. ''...Shujaa tunakuamini sauti ya wanyonge ni wewe,
Paza sauti yako walaUchumi wakuelewe, silaha upewe,
Tetea kwenye elimu kwani Uozo ndo kibao, wanatutia Ujinga wasome watoto wao, ''

Hapa maalim anaonesha imani yake kwa Hip Hop kuwa mziki huu ndo sauti pekee ya wanyonge (voice of the voiceless), kwamba ndo mziki pekee wenye kuzungumzia maisha ya mtaa, mziki wenye kuibua yasiyozungumzwa kwenye maisha ya watu wa hali ya chini. (hapa Nash kanikumbusha sana maudhui ya nyimbo moja hivi inaitwa 'On my Block' by 2pac, anaelezea maisha A to Z ya jamii yake kupitia mic).

Nash anaikumbusha hip hop iendelee kuyasemea mambo ya ufisadi na wizi wa viongozi wetu ( wala uchumi). Hali kadhalika maalim anaiambia hip hop itetee na kuanika madudu yaliyopo kwenye elimu yetu ya bongo maana sekta hii imejaa uozo (wizi wa mitihani, kufoji vyeti, n.k).

N.B: SHUJAA = HIP HOP = NASH.

CC Keyon

-Kaveli-
Heshima kwako Mkuu!

Safi sana Umefanya uchambuzi swafi kabisa na maridadi..naunga mkono uchambuzi wako.
Hakika hip hop inafikirisha ubongo wa mwanadamu!

Nash mc-mc pekee mwenye V.V.U

SHUJAA= HIP HOP =NASH MC

"Hip hop is a voice for voiceless poor people".

Umetisha Mkuu -Kavel-
 
Back
Top Bottom