Nash MC, kwanini asipewe tuzo kwa darasa hili?

Nash MC, kwanini asipewe tuzo kwa darasa hili?

'ONGEA NA MWANAO' ni wimbo bora kabisa kimaudhui katika bongo hip hop, kutoka kwa maalim Nash. Anaikumbusha jamii kuhusu malezi ya mtoto.

Wimbo huu ni ndani ya package ya Album yake iitwayo 'VITASAMOTO' released mwaka jana 2020.

Tumuunge mkono maalim Nash aendelee kutuburudisha huku tunapata dar'sa.

Unga mkono kwa kununua kazi zake.

Ukihitaji kununua albums zake, mcheki kupitia WhatsApp: 0769522346 ; 0787639655.

-Kaveli-
Namcheck faster ni muunge mkono mwanangu wa damu
 
Mashairi mazuri, uimbaji mzuri pia. Hakika anaitendea haki kazi yake

Ni emcee mahiri sana ila bado jamii imemzibia masikio. Wachache tunamuelewa Maalim Ponda a.k.a Nash Dagama.

-Kaveli-
 
Hip hop ilizaa Bongo Fleva lakini cha ajabu Bongo Fleva wamewaovertake wasanii wa hip hop ukiangalia trending hip hop mashabiki tupo wengi lakini tumefunikwa na wadosho wakata viuno keep hiphop alive, keep it real
 
Hivi bongo mziki wa hiphop inafeli wapi
Mbn hawa wakata mauno wanatawala

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app

Nadhani tatizo linaanzia kwenye mainstream media. Jamii kubwa imekuwa brain-washed na mziki wa mapenzi mapenzi tu.

Vibopa wanaocontrol media industry bado hawajataka kuipromote hip hop kwa jamii.

TV station ama radio station yaweza pitisha week nzima haijapiga wimbo wa hip hop hata mmoja.

Miaka ya nyuma angalau some TV stations zilikuwa na flatforms za kupromote huu mziki. Mfano 'hip hop base' by EATV, 'Sikia Michano' by TV1. But nowadays hakuna vitu kama hivyo kwenye media zetu. Tumebakia kusikilizishwa ugoro wa kina Gigi Money 'Nampa Papa' au kina diamond and co 'Mwanza Nyegezi'. Hujakaa sawa unasikilizishwa 'Acha lizame' by Nandy.

Mziki conscious wa kuijenga jamii umebakia kwenye social media tu kama YouTube n.k

-Kaveli-
 
Hip hop ilizaa Bongo Fleva lakini cha ajabu Bongo Fleva wamewaovertake wasanii wa hip hop ukiangalia trending hip hop mashabiki tupo wengi lakini tumefunikwa na wadosho wakata viuno keep hiphop alive, keep it real

Vibopa walioteka media industry bongo bado hawana utashi wa kuipromote hip hop.

Jamii ipo brainwashed na fleva za wabana pua tu.

-Kaveli-
 
Siku hizi napata tabu sana kusikiliza radio mziki umekua wa hovyo sana

Nyimbo za siku hizi huwezi kusikiliza wala kutazama mbele ya mama au wakwe. Nyimbo zimejaa matusi na maudhui ya kingono tu. Na ndizo zinapewa airtime ya kutosha!

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom