Uchaguzi 2020 Nashangaa sijamsikia Lissu, Magufuli wala Lipumba 'wakilisemea' hili ila huyu Mwanamke 'amelisemea' vyema mno

Uchaguzi 2020 Nashangaa sijamsikia Lissu, Magufuli wala Lipumba 'wakilisemea' hili ila huyu Mwanamke 'amelisemea' vyema mno

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Lakini TFF lazima niifute kwanza, ninawaomba Watanzania mnipe ridhaa yenu nikaifute TFF ndio inayotuletea migogoro, hizi timu zetu zisingekuwa na migogoro, mara migogoro na wawekezaji mara migogoro na wachezaji lakini chanzo ni wao".Cecilia Mmanga.

ITV Tanzania

Japo Rais wa TFF Wallace Karia ni Simba Sports Club Mwenzangu, ila 'ninaichukia' TFF kwa 'Kuzibeba' waziwazi Simba na Yanga hadi wanaharibu.

===

MMANGA: NITAVUNJA UONGOZI WA TFF, NITAKINUA SOKA LA WANAWAKE

Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Demokrasia Makini, Cecilia Mmanga amesema chama chao kinajali michezo na jambo la kwanza kufanya ni kuvunja uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)

Amesema atafanya hivyo kwa kuwa uongozi wa TFF ndio wanaoleta migogoro kwa sababu haiwezekani mchezaji mwenye mkataba akahamia timu nyingine na ukaacha tu

Pia amesema atainua mpira wa miguu kwa wanawake kwa kuwa hivi sasa mpira wa miguu umetoa kipaumbele kwa wanaume. Pia amesema watatoa kipaumbele kwa michezo mengine

Amesema watafufua hata mchezo wa Bao na kufundisha watoto kwa kuwa unatumia hesabu nyingi, Lakini amezungumzia zaidi mpira wa miguu kwa sababu unaangaliwa na wengi
 
Mmh Mag is fucked up in the head now.
Sidhani kama kwa 'Great Thinker' wa kweli tena kutoka hapa 'JamiiForums' anaweza Kukosa 'Ustaarabu' na 'Kutukana' namna hii. Pumbavu kabisa!
 
Sidhani kama kwa 'Great Thinker' wa kweli tena kutoka hapa 'JamiiForums' anaweza Kukosa 'Ustaarabu' na 'Kutukana' namna hii. Pumbavu kabisa!
Kwa akili yako fupi umeona nimetukana ila kwa lugha yetu ya kigenge nimeweka doubt.
 
..nadhani serikali ikiifuta TFF tunaweza kuingia ktk mgogoro na FIFA.

..inaweza kupelekea Tz kufungiwa kushiriki ktk mashindano ya soka ya kimataifa.
 
..nadhani serikali ikiifuta TFF tunaweza kuingia ktk mgogoro na FIFA.

..inaweza kupelekea Tz kufungiwa kushiriki ktk mashindano ya soka ya kimataifa.
UtapiaPesa tuu, hao viongozi hawajichagui.
 
Zifute Simba na Yanga uone mpira utakavyokua Tanzania. Tunadumazwa na hizi team mbili lakini ingekuwa watu wa Kigoma wana team yao wanaipenda sisi wa Kimara tuna Kimara United wa Kigamboni wana team yao tungekuwa mbali.
 
wewe kura yako ni kwa magufuli umeshafanya maamuzi na ukafungua uzi kabisa sasa unawasikiliza wengine wakusaidie nini wewe mammalia?
 
Back
Top Bottom