Nimetoka kuangalia movie inayoitwa 'Tears of the sun' ya Bruce Willis iliyotafsiriwa na huyu DJ Mac wa Acheche Production, hakika tafsiri yake ya udini ameitia chumvi mno.
Yaani kila baada ya maneno matano sita, anataja ugomvi wa kidini kitu ambacho hata movie yenyewe haisemi hivyo; anaongopa yaani.
Maneno ya humo ni makali na yanayoweza kuchochea chuki kwelikweli ya kidini. Ikizingatiwa kuwa wapenzi wakubwa wa hizi movie zilizotafsiriwa ni watoto wanaohitaji kusikia upendo na wasiohitaji kusikia maneno ya kiuaji sababu ya dini.
Nashauri sasa BASATA iwe inapitia pia hizi movie kama inavyopitia nyimbo za kina ney wa mitego ili waweze kuzuia baadhi ya mambo yasiyo sahihi.
Nawasilisha.