Nashauri China itengwe! Ugonjwa wa Chikungunya walipuka nchini humo, visa 7,000 vyaripotiwa. Marekani yatoa onyo

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Kwanini China kila ugonjwa mbaya unaanziaga huko? Baada ya COVID sasa umekuja huu mwingine unaitwa Chikungunya na kuna watu 7,000 tayari wameathirika.

Mnaonaje China ikatengwa ili mambo yasiwe mengi?

==============================================

Zaidi ya kesi 7,000 za virusi vinavyosambazwa na mbu aina ya chikungunya zimeripotiwa mkoani Guangdong, China tangu Julai, na kupelekea kuchukuliwa hatua zinazofanana na zile za Covid-19.

Mji wa Foshan umeathirika zaidi, ambapo wagonjwa wanalazimika kulazwa hospitalini chini ya neti za mbu na wanaachiwa tu baada ya kupimwa na kukutwa hawana virusi au baada ya kukaa wiki moja.

Chikungunya husambazwa kwa kuumwa na mbu aliyeambukizwa na husababisha homa kali na maumivu ya viungo yanayoweza kudumu kwa miaka.

Hong Kong imeripoti kisa chake cha kwanza, mtoto wa miaka 12 aliyepata dalili baada ya kusafiri Foshan. Virusi havisambazwi kati ya watu moja kwa moja bali kupitia mbu.

Maafisa wamesema wagonjwa wote wana hali ya kawaida, na 95% wamepona ndani ya siku saba. Hata hivyo, hali hiyo imesababisha taharuki nchini humo huku Marekani ikiwataka wasafiri kuchukua tahadhari zaidi.

Source: BBC News, Euro News
 
Naomba link ya hio habari Katika BBC news
 
Tunaomba serikali ya Tz iingilie kati
 
Kheeee mbona ngunyaa tenaa... kuna uhusiano gani na kwenda chooni
 
Jina la kikwetu na kuelezea nchi za sauzi kama

Kutoka mtandaoni haya chini
 
Ugonjwa mbona una jina la kinewalanewala au kusini kusini.
 
Huo ugonjwa mbona sio mgeni hapo kwenu Tanzania huwa unasumbua sana, ni viral disease dalili yake kubwa ni maumivu ya viungo vya uzazi na joto kali la mwili na hauna Tina maalum.
 
China ni rafiki zetu hatuwezi kuwatenga
 
Baadaye wachina watasema chikungunya ilipelekwa uchina na Raia mmakonde kutoka Tanzania au Msumbiji.
 
M
MbOna jina kama lakisuma ilo una uhakika ni china kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…