Nashauri elimu na afya ziingizwe kwenye Wizara za Muungano

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Katibu inaweza kubadilishwa kwa manufaa ya taifa. Ushauri wangu, Zanzibar hainufaiki kwa elimu na afya kwasababu ya udogo wake. Tanzania bara tuna nufaika na kutumia mbinu zinazofanana kuanzia kujenga shule, maabara, hospitali na vyuo vya afya.

Wenzetu wa Zanzibar wanapata shida maana hizi wizara zinanufaika kwa ukubwa kuanzia manunuzi ya dawa, vifaa na hata mikataba. Sijaona sababu ya msingi ya hizi wizara kuwa tofauti. Kama kuna sababu za msingi tujulisheni na tujadili hapa.
 
Awamu hii Zanzibar inafaidi Sana, mipesa kedekede inamwagika huko. Haijalishi ni kwa kazi za muungano ama zisizo za muungano ni mifweza tu.
 
Wazanzibari hawapendi kabisa hata mambo ya muungano (Union Matters) yalivyokuwa mengi hivi.
Kwanini wewe utake mengine yaongezwe ilhali mpaka sasa huu muungano ni shubiri kwa wengi ?
 
Huu muungano sijui ila inavyoonesha baada ya miaka kadhaa unaweza kufa ndio hapo kila mtu atapo kula 50 zake tubaki na Tanganyika yetu,,
 
Katibu inaweza kubadilishwa kwa manufaa ya taifa. Ushauri wangu, Zanzibar hainufaiki kwa elimu na afya kwasababu ya udogo wake. Tanzania bara tuna nufaika na kutumia mbinu zinazofanana kuanzia kujenga shule, maabara, hospitali na vyuo vya afya.

Wenzetu wa Zanzibar wanapata shida maana hizi wizara zinanufaika kwa ukubwa kuanzia manunuzi ya dawa, vifaa na hata mikataba. Sijaona sababu ya msingi ya hizi wizara kuwa tofauti. Kama kuna sababu za msingi tujulisheni na tujadili hapa.
Elimu ya juu na A level ni masuala ya muungano.
Bado p/school na O level.
 
Back
Top Bottom