Kiukweli naona nchi yetu imeanza kuwa tofauti na jinsi ilivyokua miaka ya nyuma, yani inafika muda watu wanatafuta pointi ndogo/kubwa kuanzisha taharuki katika jamii.
Nimepita katika mitandao ya kijamii watu wamekasirika na kutuhumu kuwa taifa linagawanywa kidini kwa sababu ya alama ya msalaba iliyo katika jezi ya timu ya taifa.
Kama nchi tumefikia hatua ya kuanza kugawana namna hii? Hii chuki imeanzia wapi maana inafikia watu wanatoa maoni kuwa kesho ni Msalaba 0- Uganda 4
Tanzania inaelekea wapi aisee?
View attachment 1052312
Sent using
Jamii Forums mobile app