Nashauri Jesca Kishoa asivunje ndoa sababu ya Siasa...!

Nashauri Jesca Kishoa asivunje ndoa sababu ya Siasa...!

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Nlisoma maelezo ya mtu mmoja kumtaka mbunge wa chadema avunje ndoa baada ya mumewe kuhamia ccm. Nlishangaa zaidi kuona kuna watu wanaunga mkono jambo hilo.

Ndoa siku zote hubak kuwa ni makubaliano ya watu wawili tu ambao sababu zao za kukubaliana na kuish pamoja wanazijua wao. Siasa itabaki kuwa siasa kama ambavyo kuna watu wameoana wakishabikia simba na yanga.

Sasa huyu mtu asiye na ufaham anawezaje mshawishi mwenzie avunje ndoa sabab mumewe kahamia ccm? Hii ni akili ya wapi?kwan walioana kwa minajiri gan? Kama ni wakristo ndoa zao huwa ni ngumu zaidi.maana wao hutenganishwa na kifo. Huwez sema mumeo au mkeo kahamia chama flan basi hafai tena kuwa mumeo au mkeo

Kuoana si kuchukuliana akil na ufaham. Bado kila mtu atabaki na utashi wake na ndo maana kwa mimi siwez mwambia mtu abadili dini ili nimwoe. Kama mtu anabadili dini aamue kwa utashi wake otherwise abak na dini na bado tuoane kwa makubaliano fulan.

Unaweza mshawishi mwenzio aachane na mumewe au mkewe sababu ya siasa ni sababu hujui maana ya ndoa. Kwenye ndoa mnaweza pingana lakini mwisho wa siku mnasupportiana katika jambo la msingi hamwez pingana hadharani.

Na bado kitendo cha jesca kishoa kufanya press conference kumsema mumewe alikosea sana kwa tamaduni za ndoa na malezi mazuri. Kumsema mumeo mbele za watu kuwa ni mwanaume asiye na msimamo ni ukosefu wa adabu wa kiwango cha juu.

Mwanamke mwenye hekima angesema tu hayo ni maamuzi yake yeye kafulila hayahusiani na yeye mke. Then maswali mengine aulizwe yeye mhusika. Kwa kafulila kuhamia ccm hajavunja katiba ya nchi na hajavunja katiba ya chadema. So why jesca asumbuliwe?kuonekana na mumewe hotel ni jambo jema kabisa nami nasisitiza wanapokuwa wao wawili wabak kama mke na mume na wanapokuwa kwenye siasa watabak kuwa wapinzani wa kisiasa.

Kinyume na hapo tusije siku moja tukahoji inakuaje jesca amepata mimba ya david kafulila wakati kafulila ni ccm. Tutenganishe ndoa na siasa. Tutenganishe hisia na siasa.
 
Nazani yeye ndio anamfahamu aliyemuacha,,,,nitashangaa kama wewe utauliza hivyo na kuwa na mashaka na wewe. ivi wewe ni mke au mme?
 
Wanashindwa kutofautisha ndoa na mambo mengine,kafulila na mkewe walifunga ndoa kanisani na walikula kiapo mbele ya madhabahu sio mbele ya mwenyekiti wala mbele ya lema,ni ukarai tu ndo utakwambia kwa sababu mume amehamia chama kingine basi muachane,kwani walipokuwa wanafunga ndoa kafulila alikuwa NCCR na mkewe alikuwa CDM lakini mbona hawakusema wasioane,yaani hawa jamaa wameishiwa sera wanaokoteza matukio tu ndo waende nalo
 
Ulianza Upendo ndio ikaja Siasa hivyo Siasa haiwezi kuvunja Ndoa iliyojengwa kwa Upendo, ikitokea hivyo basi juwa kuna sababu nyingine ila Siasa imetumika kama justification..,
 
Ili dunia ipate pa kuzungukia lazima wavunje tu hamna namna
 
Tofautisha siasa za enzi hizo za Dr Slaa na Rose Kamili, siasa za awamu hii ni uadui, uhasama, kupotezana, kufilisiana, kubambikiwa uhujumu uchumi n.k, kwa hali ilivyo ni ngumu Kafulila (CCM) na Jesca (CHADEMA) kuendelea kuwa pamoja, vinginevyo ni usaliti kwa upande mmoja, waamue kusuka au kunyoa wataeleweka kuliko kufanya unafiki, ndoa au siasa basi.
 
Do you mean like Mr Kafulila sasa ni eligible!!amwache tyu wiki ndefu mbona anaoa.
 
Back
Top Bottom