Nashauri: Kuongea Kiingereza kwa unyoofu (fluency) ibaki kuwa kigezo cha kumpima Mtanzania mwenye Degree

Aiseeh! Kwahiyo nikifahamu kingereza tu nami najitapa nina degree.

Anayefahamu anifundishe please,Nitamlipa.l..ani PM .

"Godu morningi sa"
Mbwembwe zangu huwa zinaishia hapa,nataka nielewe zaidi ya hapa.
Unatia mihuri elimu yako kwa kuwa na uwezo wa kuileza kwa maneno na kwa maandishi kwa lugha uliyotumia kujifunza.

Hii ndio hoja. Kujua kiingereza sio degree
 
Kabla ya Uhuru kiingereza kilianza kufundishwa kwenye shule za msingi zote nchini, yaani mtoto anafika darasa la nne anajua kiingereza ukizingatia mtoto ni rahisi kujifunza lugha kuliko mkubwa. Baada ya Uhuru ilipoletwa siasa ya ujamaa ambayo ilikuwa na lengo la kuleta matabaka, elimu ikavurugwa kukawa na eti hakuna kupasi mtihani kukiwa na lengo la kuwawezesha watoto wa viongozi waingie sekondari na vyuo! Hapo ndipo baadhi ya shule zikawa zinafundisha lugha ya kiingereza na nyingine mradi shule! Hizi hata walimu shida. Wenye uwezo wakajianzishia shule zao ili wauze kiingereza kilichokuwa si bidhaa bali lugha kama kilivyo kiswahili, biashara ikapata mwitikio wa kifahari eti za Kimataifa kwa kuuza lugha moja!
 
Kiingereza hakina kona nyingi. Kiko moja kwa moja kwenye point. Kiswahili kinatoa nafasi nyingi za ujanjaujanja na kukwepa maswali.
 
Kama mambo umefundishwa kwa kiingereza, unataka tukupimeje uelwa wako kwa Kiswahili😁😁😁
Kwani hayo unayoyaelewa kuhusu taaluma yako, huwezi kuyaelezea kwa lugha ya kwenu? AU unataka kuniambia, ukifundishwa kitu kwa kiswahili, basi ikifika kukielezea kwa kiingereza hutaweza?
 
Wakati wa kufundishwa gari, akiambiwa akanyake mfulumbato asilalamike..!!
 
Kwani hayo unayoyaelewa kuhusu taaluma yako, huwezi kuyaelezea kwa lugha ya kwenu? AU unataka kuniambia, ukifundishwa kitu kwa kiswahili, basi ikifika kukielezea kwa kiingereza hutaweza?
Jamii inayokuzunguka, na jamii ya kimataifa inajua umejifunza hayo kwa Lugha ya kiingereza, hivyo wanategemea ujue kuieleza kwa Kiingereza.

Pia tunaposema msomi. Ni kufahamu uliyojifunza kwa lugha uliyojifunzia huku tukiwa hatuna wasiwasi na uwezo wako wa kukieleza kwa lugha yako ya nyumbani.
 
Lazima apimwe kwa Lugha aliyojifunzia, maana hata hivyo docs nyingi zitakuja kwa kiingereza.

Kwanza Kiingereza ni lugha ya taifa. Sasa ofisi za taifa ziwe na watu ambao hawakijui ni tatizo.
 
Sawa sawa, njia zipi nitumie kufahamu kingereza ?hata salaam tu rafiki.
Hata mimi sijui. Wataalam watasaidia.
Kiingereza changu ni cha kuungaunga na mimi nimekipa deadline kinyooke. Maana ninajambo langu flani na wazungu, kwa kiingereza hiki watanipuuza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…