Nashauri Mawaziri, RC DC na DED wapelekwe Semina Elekezi kama enzi za JK. Fikiria wakati tunazungumzia Utekaji DC anadai Kuna Kitu alifanya Maporini!

Nashauri Mawaziri, RC DC na DED wapelekwe Semina Elekezi kama enzi za JK. Fikiria wakati tunazungumzia Utekaji DC anadai Kuna Kitu alifanya Maporini!

Chonde Chonde Waziri mkuu ni vema hawa Viongozi kuanzia Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya, Wakuu wa Mikoa na Mawaziri wakafanyiwa Semina Elekezi

Hii itasaidia kuondoa kutolewa kauli kinzani na vioywetu pia hali ya Ukambale Ndani ya Serikali na hata Chama itaisha

Mlale Unono 😃

Pia soma:Kuelekea 2025 - DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!
Ili tusijue ya nyuma ya pazia na yaliyomo ndani ya freezer zao ama?
 
Utekaji na upotezaji ni sera isio rasmi yq ccm kwa hiyo hata waelekezwe vipi lazima kuna maeneo watateleza na kutoa siri
 
Waende semina walipwe tena posho. Elezeni kwanza maporini mnafanya nini
 
DC na Nape wanastahili kuoandiswa vyeo kwa kusema ukweli.😅
Hao ndio haswaa wamefuzu semina elekezi.😅
Kumbuka kiapo chao.
"Nitasema Kweli Daima"
"Uwongo Kwangu Mwiko"
 
kusubiri semina elekezi ni dalili ya kutokujua wajibu wao na hivyo hawatakiwi kuwapo katika madaraka hayo. Semina elezezi za Kikwete zilikuwa ni upigaji wa pesa tu
 
Nimeshindwa tu kuelewa kwenye mapori kulifanyika nini na alihusikajehusikaje yeye kama yeye 🤣
 
Chonde Chonde Waziri mkuu ni vema hawa Viongozi kuanzia Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya, Wakuu wa Mikoa na Mawaziri wakafanyiwa Semina Elekezi

Hii itasaidia kuondoa kutolewa kauli kinzani na vioywetu pia hali ya Ukambale Ndani ya Serikali na hata Chama itaisha

Mlale Unono 😃

Pia soma:Kuelekea 2025 - DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!
Jo, ogopa kuua Mtu asiye na hatia. Dhambi zote fanya lakini kuondoa uhai wa mtu hapana. DC ametafunwa na dhamira na hatia.
 
Ukisikia mtu anaitwa Mwamba basi ni kama huyo Mwamba, kwanza sio muoga.
 
Mbona huwa wanaenda kupigwa msasa pale Uongozi Institute.
Shida ni kuwa CCM na serikali yake imebeba watu wabaya,watu wabaya hawajawai kuwa wazuri isipokuwa kama wanatafuta wanachotaka ndiyo hujifanya
Hii nchi km wanasema kuna vetting mie naaminndo peleka makina saini unakuta polisi anaaamriwa na muu wa wa wilaya au mkoa piga risasi hao na yeye anapiga ni upumbavu wa hali ya juu
 
Ni tabia tu ya mtu lakini semina huwa zinafanyika mara nyingi sana za masuala mbalimbali Mtambuka ikiwepo hilo unalolitaka wewe. Mara ngapi umesikia kupitia vyombo vya habari viongozi hao wakiwa katika semina.

Kumbuka tabia ni kama Ngozi tu.Wengine unawapa semina leo halafu kesho anafanya kilekile alichokatazwa jana. Ila nimesikitishwa sana na maneno ya Mheshimiwa DC kwa sababu amejidhalilisha sana na kuikosea heshima ofisi ya DC NA KUMKOSEA SANA Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Mwisho niseme kuwa hapa Duniani kuna watu wanachezea sana nafasi mpaka mtu unabaki unashangaa.Yaani mtu unapata Uteuzi wa Rais halafu unauletea mchezo? Mimi siwezi kufanya ujinga huo kuchezea nafasi. Watu wapo mitaani na vyeti vyao lakini hawana kazi unafikiri wanaweza kufanya kazi kiasi gani wakipewa nafasi ya uteuzi wa Rais?
Hapa leo lucas umeongea kama mzalendo sio kama siku nyingine, lakini sasa ukweli umeujua yale maneno yako ya kujibwambafy kuwa mnashinda kwa kishindo umesikia kinachofanyika sasa???? Ushauri wangu usiwe chawa kwa kila kitu ndugu yqngu mwashambwa! Naomba sasa uelekeze nguvu zako huyo dc achukuliwe na vyombo vya dola asaidie polisi huko maporini walikuwa wanafanya nini ???
 
Huyu DC wa Longido amesema Ukweli mchungu sana. Hataki Unafiki.

CCM KUENDELEA KUBAKI MADARAKANI AU KUSHINDA KWENYE UCHAGUZI HAITEGEMEI KUPIGIWA KURA NA MTU YOYOTE YULE KATIKA UCHAGUZI WA SIASA HAPA NCHINI TANZANIA.

Aidha, katika Uchunguzi uliofanyika kwa kificho ulibaini kwamba wale Watu waliohusika kwenye Usimamizi wa Uchaguzi wa Siasa hapa Tanzania Mwaka 2020 walikuwa ni aidha Mawakala wa Siri wa TISS au Maaskari Polisi. Siku chache kabla ya Uchaguzi huo Watu hao Walikusanywa kwenye Makambi kwa ajili ya kupewa Mafunzo Maalumu ya Kuhujumu Uchaguzi huo ili kuipa Ushindi CCM.
Ma-DSO wote waliokuwepo walikabidhiwa jukumu maalumu la kuratibu na Kusimamia Mpango huo.

Kwa wale Watu wengine waliohudhuria mapema kwenye Vituo vya Kupiga Kura siku ya Uchaguzi Mwaka huo wa 2020 nafikiri mtakuwa mashuhuda wazuri kwamba mliwakuta Vijana waliobeba mabegi kwenye vituo vya kupigia Kura, hao ndio Watu wenyewe waliohusika na utekelezaji wa Mpango huo
Uko sahihi 100%
 
Chonde Chonde Waziri mkuu ni vema hawa Viongozi kuanzia Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya, Wakuu wa Mikoa na Mawaziri wakafanyiwa Semina Elekezi

Hii itasaidia kuondoa kutolewa kauli kinzani na vioywetu pia hali ya Ukambale Ndani ya Serikali na hata Chama itaisha

Mlale Unono 😃

Pia soma:Kuelekea 2025 - DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!
Hata mkiwapa masemina mengi mengi bado huku mitaani na kwenye vikao vya ndani wataendelea kutamba!
 
Chonde Chonde Waziri mkuu ni vema hawa Viongozi kuanzia Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya, Wakuu wa Mikoa na Mawaziri wakafanyiwa Semina Elekezi

Hii itasaidia kuondoa kutolewa kauli kinzani na vioywetu pia hali ya Ukambale Ndani ya Serikali na hata Chama itaisha

Mlale Unono 😃

Pia soma:Kuelekea 2025 - DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!
Semina elekezi itasaidia nini ilhali waliopewa nafasi hizi ni majambazi?! Mtekaji yeyote ni jambazi awe ofisini au mtaani.
 
Back
Top Bottom