Nashauri mechi ya derby ichezeshwe na refa kutoka nje

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Hii mechi ya ngao ya jamii tarehe 8 ingetakiwa TFF na bodi ya ligi wamlete refari kutoka nje ambaye ana uzoefu mkubwa ili kuepuka lawama na kasoro za upendeleo wa wazi kama wanavyofanyaa marefa wa ndani hasa Kayoko na Arajiga, inashindikana nini mbona mechi ya Al Ahly na Zamalek ilikuwa ichezeshwe na refa kutoka nje.
 
Kwa hii nchi ya kuabudu uzalendo uchwara na Uzawa na kufurahisha wanasiasa na wakuu hilo haliwezekani, Tena kwa kutaka kumfurahisha mama yao wanaweza kumpa mwanamke ndo achezeshe

Soka letu Siasa Nyingi Sana
 
Umewataja kina Arajiga na yule mama Tatu mbona humtaji?
 
 
Kama Tff na Bodi ya ligi wanataka kuifanya dabi ya Simba na Yanga iwe na thamani walete marefa kutoka nje na sio Hawa wetu wanaochezesha kwa maelekezo.
Aragija kachezesha mfululizo lakini Hana improvement yoyote zaidi ya kuongeza madudu.
Kuna yule refa muethiopia na marefa wengine waafrika wanaochezesha world cup wanaweza kuwachukua.
Ukiona mtu qnapinga maamuzi ya refa kutoka nje ujue timu yake ni mnufaika.
 
Kuna mechi ya Al Ahly na Zamalek ilikuwa ichezeshwe na refa kutoka Spain kama sikosei,ila Zamalek waligoma kucheza kisa Al Ahly wana viporo vingi . Inaonekana inawezekana kabisa kuwa na refa kutoka nje kwa ajili ya mchezo wa derby,tunaona kabisa hata hawa marefa wanaochezesha club bingwa walivyo wazuri
 
Marefa wenye uwezo na uzoefu wapo halafu kuna VAR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…