Nashauri msemaji ya Tabora united asibugudhiwe, ila ataniwe TU

Nashauri msemaji ya Tabora united asibugudhiwe, ila ataniwe TU

Ni mental case. Anakuambia eti huu msimu utakua wa mwisho kuifunga tabora. Nikajua hii ni mental case tu
Ha ha haa,yaani alivyopiga u turn ghafla utashangaa.
Wakati hata yeye Hana uhakika huko mbele hajui kama atakuwepo siku Simba ikicheza Tena na Tabora.
 
Huyu ni dada yetu, ni mpenda soka mwenzetu, na anaifanya soka ipendwe zaidi na wanawake/wasichana.

Naomba wanaume wenzangu kwa vyovyote vile mtanieni utani wote lakini nawashauri msimtanie utani usio faa, usio katika maadili ya taifa letu na hususan msimtanie mambo yanayokwaza kwa jinsia yake.

Maana nimesikia Kuna baadhi ya wanaume wamekua wakimkashifu kuhusiana na jinsia yake.

Fifa imelifanya soka kua mchezo wa wote naomba tuheshimu hilo.

Ila kaeni mkijua kua Kuna familia baba Simba mama Yanga na kinyume chake,watoto yanya wengine Simba na tofauti na wazazi wao.

Mfano Ali Kamwe ni Yanga baba yake ni Simba,pia fahamuni kua Ahmed Ali na Ali Kamwe ni marafiki wakubwa sana.

Nimeamua kueleza hivyo baada ya kuona Kuna baadhi ya wanaume wanamshambulia Christina wa Tabora kwa jinsia yake badala ya kumcheka kama msemaji wa Tabora UNited.

Kwa wanasimba wenzangu kumbukeni kua tuna timu yetu ya wanawake Simba Queens, inatoa adhabu kali sana Kwa timu nyingine za wanawake zinazojichanganya kwake.

Soka Sasa hivi limekua,kumpata msemaji wa kike kama Christina ni furaha sana.

Naomba tumpe heshima yake lakini tuendelee kumcheka kwa kuponzwa na "kamdomo"
Simba 3-0 Tabora,
Simba guvu mpya😄
I🦁🦁🦁
Anaongea kwa tungo tata
 
Amejua kuitumia Simba kupaisha jina lake.
Sasa hivi anajulikana Afrika nzima kwa kujaribu kuitishia Simba,akili mkichwa.
Nimejikuta nampenda TU ghafla,hata Ahmed Ali kamsifia na amepelekea kujaza nyomi uwanja wa Ali Hasan Mwinyi.
Fo sure...kaitumia vzr fursa ya mnyama
 
Back
Top Bottom