Nashauri Salamu ya “Shikamoo” watoe watoto chini ya Miaka 16. Inaonekana wakubwa wengi hawaipendi

Nashauri Salamu ya “Shikamoo” watoe watoto chini ya Miaka 16. Inaonekana wakubwa wengi hawaipendi

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,850
Reaction score
6,030
Hili Suala la Hii Salam ya Shikamoo limekuwa na Ukakasi Kidogo, watu wengi katika makundi ya watu wazima, wazee, na vijana wa makamo wamekuwa hawapendi salamu hii zaidi na zaidi , makundi haya ya watu huwa hawapendi kusalimiwa na makundi ya watu wakubwa wenzao mfanyo mzee kusalimiwa na mtu wa makamo, mtu wa makamo kusamiliwa na kijana mtu mzima.

Ni Salamu ambayo mtu akipewa na mtu mzima anaona ni kama kaambiwa usha expire, ila cha cha ajabu makundi yote niliyoyataja wamekuwa wakipokea salamu hizi kutoka katika kundi la watoto bila tatizo lolote, na wamekuwa hawana shida na kupokea salamu hizo, na hili limenipelekea kufikiria kuwa salamu ya shikamoo wawe wanatoa watoto chini ya miaka 16 tu, na salamu hizi zitatolewa kwa watu waliowazidi umri kuanzia angalau miaka mitani(5).

Sijui asili ya salamu hii ni nini, na mashangazi hasa watu wanene wamekuwa hawapendi kuambiwa shikamoo kwakuwa wanaona kama ni tusi la kuambiwa umechoka
 
Mkisha iua hiyo Salaam ya Shikamoo, kifuatacho ni kuua Salaam za makabila yenu.
 
Back
Top Bottom