Nashauri Salamu ya “Shikamoo” watoe watoto chini ya Miaka 16. Inaonekana wakubwa wengi hawaipendi

Nashauri Salamu ya “Shikamoo” watoe watoto chini ya Miaka 16. Inaonekana wakubwa wengi hawaipendi

Ni salamu ya kitumwa, mimi salamu hii siipokeagi hata siku moja. Ni kama kuenzi utumwa.
 
Ni kweli,mim sahv namsalimia yule mwenye makunyanzi usoni yaan kikongwe lakin hawa wenye miaka 50 kushuka chini nawapa habari za sahiz ingawaje watu wengine niliozoeana nao huwa wananizingua nikiwa nao
 
Salamu ya shikamoo siipendi hasahasa kwa wanawake maana wengine unamuona ni mkubwa sana kumbe ana miaka 30 tu,mwingine unamuona kama mdogo kumbe ana miaka 40
 
Hii salamu tumeirithi toka ukanda wa pwani, sie bara tulisalimiana kwa lugha zetu.
 
Tukae humu ..assalam alaikum kama wenzetu waliostaarabika nchi jiran Chake chake.
Hii salaam ni rahisi, meaningful na genderless.
Kuliko hii ya kitumwa ya ..niko chini ya miguu yako! (sijui unafanyako nini).
Tatzo mbumbumbu wanadhan asalam... ni salaam ya kiislam.
Kuiga chema si ushamba!
Salaam aleykum na Uislamu ni mapacha walioungana kifuani na wanatumia moyo mmoja. Kuwa tenganisha haiwezekani.
 
Hili Suala la Hii Salam ya Shikamoo limekuwa na Ukakasi Kidogo, watu wengi katika makundi ya watu wazima, wazee, na vijana wa makamo wamekuwa hawapendi salamu hii zaidi na zaidi , makundi haya ya watu huwa hawapendi kusalimiwa na makundi ya watu wakubwa wenzao mfanyo mzee kusalimiwa na mtu wa makamo, mtu wa makamo kusamiliwa na kijana mtu mzima.

Ni Salamu ambayo mtu akipewa na mtu mzima anaona ni kama kaambiwa usha expire, ila cha cha ajabu makundi yote niliyoyataja wamekuwa wakipokea salamu hizi kutoka katika kundi la watoto bila tatizo lolote, na wamekuwa hawana shida na kupokea salamu hizo, na hili limenipelekea kufikiria kuwa salamu ya shikamoo wawe wanatoa watoto chini ya miaka 16 tu, na salamu hizi zitatolewa kwa watu waliowazidi umri kuanzia angalau miaka mitani(5).

Sijui asili ya salamu hii ni nini, na mashangazi hasa watu wanene wamekuwa hawapendi kuambiwa shikamoo kwakuwa wanaona kama ni tusi la kuambiwa umechoka
Kanda ya ziwa wanaipenda sana salamu tajwa😂😂😂
 
Kama umeweza kumiliki na kuhudumia familia mjini wewe mwenyewe, unatoa shikamoo ili ikusaidie nini? Kwamba itakuletea chakula?​
 
Siku hizi ni kawaida kukutana na bibi wa miaka 60 anakuambia habari za sahizi hii salamu wengi sasa hawaitaki
 
Back
Top Bottom