Nashauri Salamu ya “Shikamoo” watoe watoto chini ya Miaka 16. Inaonekana wakubwa wengi hawaipendi

Ni salamu ya kitumwa, mimi salamu hii siipokeagi hata siku moja. Ni kama kuenzi utumwa.
 
Ni kweli,mim sahv namsalimia yule mwenye makunyanzi usoni yaan kikongwe lakin hawa wenye miaka 50 kushuka chini nawapa habari za sahiz ingawaje watu wengine niliozoeana nao huwa wananizingua nikiwa nao
 
Salamu ya shikamoo siipendi hasahasa kwa wanawake maana wengine unamuona ni mkubwa sana kumbe ana miaka 30 tu,mwingine unamuona kama mdogo kumbe ana miaka 40
 
Hii salamu tumeirithi toka ukanda wa pwani, sie bara tulisalimiana kwa lugha zetu.
 
Salaam aleykum na Uislamu ni mapacha walioungana kifuani na wanatumia moyo mmoja. Kuwa tenganisha haiwezekani.
 
Kanda ya ziwa wanaipenda sana salamu tajwa😂😂😂
 
Kama umeweza kumiliki na kuhudumia familia mjini wewe mwenyewe, unatoa shikamoo ili ikusaidie nini? Kwamba itakuletea chakula?​
 
Siku hizi ni kawaida kukutana na bibi wa miaka 60 anakuambia habari za sahizi hii salamu wengi sasa hawaitaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…