#COVID19Nashauri Serikali iandae mdahalo mubashara wa Television baina ya Askofu Gwajima na Waziri wa Afya ili kumaliza utata uliopo juu ya usalama wa chanjo
#COVID19Nashauri Serikali iandae mdahalo mubashara wa Television baina ya Askofu Gwajima na Waziri wa Afya ili kumaliza utata uliopo juu ya usalama wa chanjo
Utafiti mpya uliofanywa na Kituo Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) unaeleza kuwa chanjo ya Covid-19 bado ina umuhimu mkubwa katika kudhibiti homa kali na vifo vinavyotokana na Covid-19. Aidha, inaelezwa utafiti huo ulichunguza visa 600,000 kutoka katika Majimbo 13...
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali inaandaa utaratibu wa wiki ya uchanjaji ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzoni mwa mwezi Oktoba. Msigwa ameyasema hayo Jumapili Septemba 12, 2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya wiki. ''Serikali moja ya...
Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) linasema ni vyema watu wazima wakawa na taarifa sahihi kabla ya kuzungumza kuhusu chanjo ya COVID-19 na watoto Inashauriwa pia kusikiliza maoni na mitazamo yao na kuzingatia hofu zao Ni vema wakaona wapo huru kueleza mitazamo yao kwa watu wazima...
Dar es Salaam. Katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19, waganga wakuu wa mikoa wameishauri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, iangalie uwezekano wa kuifanya chanjo ya ugonjwa huo kuwa ya lazima. Wito huo wameutoa, kufuatia vifo vinavyoendelea kuwakumba...
Huyu ni mhudumu wa afya toka Italia. Msikilize naamini utajifunza jambo. Dunia imedanganywa tangu Desemba 2019. Na inaendelea kudanganywa. ……….. Anasema: Habari, Mimi naitwa Cristina. Ni mhudumu wa afya, Na nilitaka kumjibu Andrea Mandelli Kwa hiyo bwana Mandeli Umeongelea ukweli kwamba Vyumba...
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Tanzania inatarajia kupokea Dozi Milioni 2 za Sinopharm kutoka Nchini China. Kwenye chanjo hiyo, mtu atapokea dozi mbili tofauti na Johnson & Johnson ambayo inachomwa mara moja Akizungumza kutoka Mkoani Singida, Msigwa ameeleza kuwa idadi ya...
Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima ameliagiza Baraza la Madaktari (MAT) kuwachukulia hatua madaktari watakaotoa taarifa potofu kuhusu ugonjwa na chanjo dhidi ya UVIKO19. Amesema atakayeshindwa kuthibitisha taarifa zake atachukuliwa hatua, lengo likiwa ni kudhibiti upotoshaji.
Wizara ya Afya imetoa ufafanuzi wa kina kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo chanjo ya COVID-19. Tazama uone namna chanjo inafanya kazi na masuala mengine muhimu. Je, Vijana wanaweza kulazwa kwa Covid-19 DKT. ISAAC MARO: VIJANA HUWEZA KULAZWA AU KUFARIKI KWA #COVID19 Daktari Isaac Maro...
Mdahalo wa wazi hutumika hata kule Marekani kipindi cha uchaguzi, ambapo wagombea kupitia vyama pinzani huwekwa kwenye jukwaa moja na kupitishwa kwenye ‘tanuru la moto’ ili kuona nani anafaa, vivyo hivyo ifanyike kwa Askofu Gwajima na Waziri wa Afya (Serikali) ili tuweze kupata ‘consensus’ ya kitaifa juu ya usalama wa chanjo ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu.
Hoja ambazo wengi tuna shauku ya kuona zikijadiliwa , baadhi ni hizi:-
1.) Je, madhara (side effects) ya muda mfupi, muda wa kati (miaka mi5) na ya muda mrefu (miaka 10) ya hizo chanjo, kwa atakaechoma na kwa watoto atakaowazaa ni yapi?
2.) Je, chanjo ni nini? , yaani ili kitu kiitwe ‘chanjo’ kinatakiwa kiweze kufanya nini na nini? , na kwamba je, hicho kinachoitwa chanjo, kinaweza kufanya hayo?
3.) Kwa kuwa kirusi hiki huwa kinabadilika badilika kila baada ya muda fulani (fact), je, hii chanjo ya Johnson & Johnson iliyoletwa ni kwa ajili ya aina gani ya kirusi cha Corona, au ni kwa ajili ya aina zote za virusi vya Corona? Na kama kikija aina mpya ya kirusi, mfano ‘delta variant’ itabidi watu wakachomwe tena? Na kikija kingine wakachomwe tena? Na kikija kingine wakachomwe tena? Hadi lini? Mwisho wake ni lini?
4.) Je, tukishachomwa hiyo chanjo ya Corona, tunaacha kuvaa barakoa?, tunaweza kujichanganya kwenye mikusanyiko? , tunaweza kushikana mikono na kukumbatiana? , tunakuwa hatuwezi kupata maambukizi ya Corona? Tunakuwa hatuwezi kuambukiza wengine? Na je, ni kwanini wanaochoma chanjo wanaogopa zaidi Corona kuliko wasiochoma?
5.) Nk, Nk, Nk, Nk.
Sasa bila kujibu hizi hoja, hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuwaelewa, nasikitika hadi kiongozi mkuu wa nchi anaanguka kwenye mtego wa kujibu hoja kwa vijembe kama anavyofanya waziri wake, mnatufanya tujute kutoa nafasi za uongozi kwa usawa baina ya jinsia zote, mnawaangusha wanawake. Hivi kweli mtu anasema bila wasiwasi kwamba ametestiwa mitambo na mumewe na kwamba yupo fiti, are we serious, hoja ndio hujibiwa hivyo? Hoja hujibiwa kwa hoja.
================================ View attachment 1945727
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Tanzania inatarajia kupokea Dozi Milioni 2 za Sinopharm kutoka Nchini China. Kwenye chanjo hiyo, mtu atapokea dozi mbili tofauti na Johnson & Johnson ambayo inachomwa mara moja Akizungumza kutoka Mkoani Singida, Msigwa ameeleza kuwa idadi ya...
Jaribio la wanasayansi kubaini dawa ya homa ya Uviko-19 linaelekea kuzaa matunda baada ya kuwapo kwa taarifa za matumaini makubwa vidonge vya ‘Molnupiravir’ kufanya kazi kwa ufanisi kutibu ugonjwa huo. Dawa hiyo iliyofanyiwa majaribio na kampuni ya kimataifa ya kutengeneza dawa ya Merck iliyopo...
Kufuatia ripoti kuhusu Watoto kukimbia Shuleni, Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima amesisitiza Chanjo dhidi ya COVID19 zitatolewa na wenye umri wa zaidi ya miaka 18 pekee Ameeleza, "Hakuna mtoto aliye chini ya miaka 18 ambaye atachanjwa. Na hawa wa miaka 18 na kuendelea watachanjwa kwa hiari...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.