Nashauri serikali ianzishe route za daladala zinazo zunguka duara bila kurudi nyuma pia daladala zipewe namba maalumu ili zitambuliwe na abiria

Mtu yupo mwananchi anataka kwenda mawasiliano, hapo atapanda gari gani?
 
Mkuu sidhani umenielewa vizuri....... Mbezi- Makumbusho kuna magari ya route mbili,na yote yanapishan barabarani
 
Imagine uko Tabata Bima unataka kwenda Mwananchi itabidi uzunguke hadi Mawasiliano uanze round kurudi Mwananchi. Upotevu wa muda na fedha maana nauli itakuwa kubwa kwasababu ya mzunguko mrefu ilhali uendapi ni karibu sana.
 
Imagine uko Tabata Bima unataka kwenda Mwananchi itabidi uzunguke hadi Mawasiliano uanze round kurudi Mwananchi. Upotevu wa muda na fedha maana nauli itakuwa kubwa kwasababu ya mzunguko mrefu ilhali uendapi ni karibu sana.
Hapana mkuu yaani route zitakua nyingi sana. Kuna daladala zingine zitapita hapo Tabata Bima zikitokea Gongo la Mboto au Segerea. Route zitakua nyingi ila daladala zitakua hazirudi nyuma. Zitakua nyingi tu mkuu.
 
Una wazo zuri Sana ila kama Tu mwendokasi mwenye njia Yake Yuko vile hizo gari sasa zitakuwaje?
2.Bongo bado ni developing country hatujafikia level hizo za developed country
 
Ngoja tuone...
Route zitakua ndefu sana kwa hizi barabara zetu...


Cc: Mahondaw
Route hazitakua ndefu. Chukulia mfano daladala inatoka Mwenge Mpaka Buguruni inarudia route hiyohiyo mara mbili. Sasa ukaamu kuipa hiyo daladala namba 709 ikiwa na maana ni mojawapo ya daladala inayopita route ya Mwenge, kuelekea Mpakani, ipite Ubungo, riverside, External, Garage, Mwananchi, Tabata Reli, Buguruni, Ilala, Kariakoo, Jangwani, Magomeni, Morocco, Victoria, Mwenge. Kisha inaanza tena mzunguko Mwenge, kuelekea Mpakani, ipite Ubungo, riverside, External, Garage, Mwananchi, Tabata Reli, Buguruni, Ilala, Kariakoo, Jangwani, Magomeni, Morocco, Victoria, Mwenge.
 
Hii route ipo moja naijua ipo hivi.

mbezi> madale> tegeta> mwenge> ubungo> kimara> mbezi.

konda na dereva wanavaa mashati ya blue bahari.
Hivi ndio inavyotakiwa sasa. Na daladala zote zinazozunguka njia hii zingetakiwa kupewa namba ili zitambulike kirahisi na abiria.
 
Mkuu umeeleza vizuri sana. Wasalimie hapo UK. Lakini hata hizi daladala za saivi zingepewa namba naona kama ingewezekana. Namba ni utambulisho wa daladala ili abiri aweze kuitambua kiurahisi. Mfano saivi ukisahau mzigo kwenye daladala sidhani kama unaweza kuupata kiurahisi. Lakini kama zingekua na namba ungeweza kukumbuka nilipanda daladala namba fulani ngoja nilisubiri lirudi nitaulizia mzigo wangu. Lakini kwa mfumo wa saivi daladala zote zinafanana majina. Namba plate haiwezi kutumiwa na abiria.
 
You mean namba exclusive kwa kila daladala ?!!! That is Impossible Ila kinachowezekana ni kila Route inakuwa na Namba ambapo sasa hivi kila Route ina majina (mfano Kariakoo Posta) na kuhusu kupotea ni kutokuwa na uaminifu mfano kwenye sehemu ambazo zimeendelea na mabasi yapo chini ya mtoa huduma mmoja mkubwa be it consurtium or whatever.., mzigo ukipotea unapelekwa katika lost property ofisini wewe unachofanya ni kupiga simu huko au kuufuata huko...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…