Nashauri Serikali isitishe ujenzi wa daraja la Busisi, SGR na Makao Makuu Dodoma

Nashauri Serikali isitishe ujenzi wa daraja la Busisi, SGR na Makao Makuu Dodoma

Huyo pimbi akili yake anawaza busisi tu hajui magari yanayopita hapo ni mamia kwasiku watu ndo usiseme!
Hayo magari yameanza kupita baada ya jiwe kuwa Rais? Daraja la Busisi ni upotevu wa fedha
 
hata mkisitisha miradi yote bado hali itakuwa MBAYA SANA, kwa muelekeo huu wa wafanayabiashara wakubwa kukwepa kodi na matumizi ya ovyo ya serikali...watu tunajiuliza convoy nzima iliyoambatana na rais kwenda Misri walikenda kufanya nini, hadi Ndalichako! siku si nyingi na na mishahara itakosa kwa watumishi.
Jiulize tu hata kudai risiti siku hizi hamna hamasa kabisa! Yaani aliyesema bunge la mazuzu naomba atambue hata serkali inaweza kuwa ya mazuzu vilevile!
 
Binafsi sioni tija yoyote kutumia mabilioni ya shilingi kujenga daraja kwenda Busisi. Kiuchumi hailipi. JPM alipumbazwa na upendeleo wa ukabila.
Halafu ukute wewe ni mtu wa Manushi chini huko Kibosho unakosoa ujenzi wa daraja la Busisi!!!

Dunia hii!!

Hivi watu wa huko wamelalamika kuhusu ujenzi wa hilo daraja!?
Huwezi kuujua umuhimu wa matako, mpaka siku utakalia kichwa.

Wahanga wa huko Busisi ndo wanaojua umuhimu wa hilo daraja.
 
Kwa mujibu wa Nape Nnauye nchi yetu inatumia shilingi bilioni 800 kwa mwezi kulipa madeni. Halafu shilingi bilioni 600 hutumika kila mwezi kulipa mishahara ya watumishi serikalini.

Lkn makusanyo kwa mwezi ni kati ya trilioni 1.2 - 1.3 kwa mwezi. Hivyo fedha hazitoshi kuendelea na miradi yote hiyo. Tunapaswa kama taifa kuachana na miradi mikubwa isiyo kuwa na tija.

1. Daraja la Busisi tuachane nalo kabisa. Kwasbb halitarajiwi kuleta tija yoyote ya kiuchumi hata likikamilika maana linaenda kijjjini (interior) Busisi. Mabilioni ya fedha yatapotea bure kabisa!

2. Ujenzi wa makao makuu Dodoma usitishwe hadi hapo serikali itakapokuwa na uwezo wa kifedha.

3. SGR iishie Morogoro hapo hapo panatosha. Awamu ya 8 itakuja kuendeleza kutoka Morogoro kwenda mbele.

4. Ndege zilizonunuliwa zinatosha. Ndege 5 ambazo ziko kwenye mpango wa kuongezwa ifikapo 2023 tuachane nazo.

N.B. JNHPP ndiyo mradi pekee ambao inabidi tuendelee kupambana nao kwa sasa maana karibia utakamilika. Japo kuna changamoto ya tabia nchi

Natanguliza shukurani endapo ushauri wangu utafanyiwa kazi.
Ata Daraja la Wami halina maana lisitishwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada una hoja ya msingi sana.
Kama uwezo wetu wa kukamilisha hiyo miradi uko chini, kwanini tulazimishe kukamilisha hiyo miradi?
Upande wa pili, kama hiyo miradi tumeshindwa kumudu kuikamilisha, kwanini tuanzishe miradi mingine mipya?

Nawaza tu, hivi ni kwanini Magufuli alisitisha uendelezwaji wa miradi ya Gesi ya Mtwara, Bandari ya bagamoyo, gesi ya Lindi, ujenzi wa Kigamboni city nk?
 
Sioni sababu yenye mantiki ya kusitishwa miradi hiyo yote hususani SGR, daraja la Busisi na bwawa la kufua umeme la mwalimu Nyerere kwa manufaa ya kiuchumi isipokuwa usitishwe miradi ya ununuzi wa ndege uliokusudiwa na serikali kwani zilizopo bado hazijaonyesha matunda toshelevu badala yake pesa hizo zielekezwe kwenye miradi mingine yenye tija kwa Taifa hususani zinazogusa wananchi moja kwa moja mf.kilimo na huduma zingine za kijamii.
 
Hata Busisi hupajui unapayuka hapa tù! Hivi kisa kwa wasukuma Roho zinawauma? Hujui kuwa mwanza anakua kwa kasi na inaifatia Dar kiuchumi? Au wangejenga Dar au kaskazini ungekuwa unachekelea hapa! Mbona hujazungumzia daraja la mto wami kusitiswa?

Njoo na hoja Mkuu, hizo hasira hazisaidii,
Kama kweli tulikuwa hatuna ukabila je
SGR lot 5 ilitakiwa iende wapi kati ya Kigoma na Mwanza?
Reli kuja Mwanza kuna tija kiasi gani kulinganisha kama ingeelekea Kigoma?
Hasa kama ungetangulia Utaifa na si Ukanda?
 
Kama kuna jambo linatafuna pesa za nchi kwa sasa kihuni basi ni suala la kuhamia Dodoma. Ukweli uliopo ni kuwa kwa sasa serikali imerejea Dar kinyemera (yaani Rais na watendaji wake wote wakuu wako Dar na hawapendi kuwepo Dodoma) huku watendaji wengine wengi wa serikali wakiendelea na shughuli zao za kila siku wakiwa Dar na wote wanalipwa posho kama wako nje ya Dodoma kikazi.
 
Back
Top Bottom