Papaa pedeshee
JF-Expert Member
- Nov 7, 2021
- 274
- 394
Ni ukweli usiopingika kuwa, katika kila zama za uongozi kuna mabaya na mazuri yaliyofanywa na viongozi au watawala hao. Serikali ya awamu ya 5 inaweza kuwa ndoa awamu iliyokuja na stahili tofauti ya kiuongozi katika nchi na hivyo mapungufu na madhaifu yakaonekana bayana tena yanayogusa maisha ya watu na hivyo hata yale mazuri mengi ya kuijenga nchi yakafunikwa na madhaifu japo yanaonekana.Mkuu ifike mahali wastishe kila kitu ambacho kulifanywa awam ya 5 ila waje ma genuine ambao watakuwa na vitu vipya awamu ya sita, kiukwel tumechoshwa na kusikia watu wanavyo mu- underline Mwamba,
Ushauri wangu wasitishe kila kitu, ada za shule zirudi, reli iishie hapo, madaraja makubwa yaachwe!, Cjui vyote viachwe maana awamu ya 5 haikuwa na Cha maana, kulikuwa na uonevu, ukandamizaji wa democracy, uuwaji, unyonyaji , Rushwa ilishamili, kulikuwa hakuna uwajibikaji n.k,
Wawafungulie kesi wote waliokuwepo awam ya 5, ikiwezekana adhabu ya kunyongwa iwe ndo adhabu ya juu, na hvyo nchi itakuwa salama maana watu wa haki watakuwa wameingia, ma genuine, watetz wa wanyonge, wawajibikaji, wanaojua kuendesha nchi vzr..
Ni wazi kuwa miradi iliyoanzishwa ilikuwa na iko kimkakati zaidi katika kujenga na kuimarisha uchumi wa nchi na watu wake, shida ni kuwa watendaji au viongozi wanatupeleka katika mwelekeo wa pamoja au Lah!
Uwajibishwaji wa viongozi wa umma mara nyingi unaweza kuchagizwa na viongozi au watawala waliopo madarakani lakini pia siasa kupewa kipaumbele sana hata kwenye mambo ya msingi.naunga mkono kuwajibishwa kwa waliokengeuka, lakini ni nani atamfunga paka kengele? Ahsante.