Munch wa annabelletz47
JF-Expert Member
- Aug 13, 2019
- 1,885
- 3,227
Kigezo cha kuajiriwa serikalini ni unyonyaji usio na mantiki yoyote. Kinacholenga kutufanya taifa lenye watu wengi wasio na elimu ya kutosha, hali inayokwamisha maendeleo ya kitaifa katika nyanja mbalimbali.
Vijana wenye maarifa na damu changa hukosa nafasi, na hivyo, sekta za serikali na hata binafsi hubaki mikononi mwa wazee waliochoka, wagonjwa, na wasioendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia na sayansi.
Hali hii imesababisha udumavu wa fikra na ukosefu wa maono ya muda mrefu katika taasisi nyingi. Wengi wa wabobezi wanaojaza nafasi muhimu ni watu waliokata tamaa, wasioweza kuhimili changamoto za ulimwengu wa kisasa, na ambao mawazo yao ya kizamani yanazidi kuathiri ufanisi wa mashirika na sekta binafsi.
Ni wazi kwamba nchi zinazowekeza kwa dhati kwenye elimu, kama Korea Kusini, zimepiga hatua kubwa kwa muda mfupi.
Tunapaswa kuiga mfano huo kwa kuhakikisha tunakuza kizazi chenye elimu bora, maarifa ya kisasa, na uwezo wa kutumia teknolojia kwa manufaa ya taifa.
Hii itasaidia kujenga msingi thabiti wa maendeleo endelevu na kufanikisha malengo ya kitaifa.