#COVID19 Nashauri Serikali wapike pilau na nyama pia na soda kwenye vituo vya kutolea chanjo

#COVID19 Nashauri Serikali wapike pilau na nyama pia na soda kwenye vituo vya kutolea chanjo

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Nimeona taarifa ya wizara kua chanjo itaanza kutolewa Agost 3

Nashauri Serikali yetu pendwa chini ya Rais samia, wahakikishe kwenye vituo vya chanjo kuna Chakula

Napendekeza Pilau na nyama
Upande wa nyama wenyewe kama ikiwepo ya kuku itapendeza zaidi lakini wa kienyeji au kama kuku itakua ni ghali basi ya ng'ombe

Ila kwa wale wasio kula nyama ziwepo samaki, na pia mboga za majani kama chainizi kabichi na maharage, au mchicha

Waweke na ndizi za kupikwa but waweke na wali maji maana kuna watu hawalagi pilau, mchele waangalie ule mzuri mzuri mabao sio mpya maana ndio unanukia sana hata kama upo umbali wa mita 400 unasikia harufu,

Matunda pia nashauri waweke ndizi na matikiti maji

Waweke soda na juice ili mpata huduma awe na option ya kuchagua

Mje muone kama watu hawatamsaliti Gwajima

Kila lakheri hayo ni maoni yangu binafsi kama mtaniunga mkono ipitishwe

download.jpeg
 
Kizuri kinajiuza wewe lofa, acha ujinga. Hivi mnadhani Watanzania ni wajinga kihivyo? Sasa hiyo si bait, wanaona!
 
USA wanatoa 100$ kwa kila mpimwaji[emoji16][emoji16][emoji16]

Hapa ndio wanazidi kutuvuruga sasa na hizi chanjo.
 
napendekeza Pilau na nyama
upande wa nyama wenyewe kama ikiwepo ya kuku itapendeza zaidi lakini wa kienyeji au kama kuku itakua ni ghali basi ya ng'ombe

ila kwa wale wasio kula nyama ziwepo samaki, na pia mboga za majani kama chainizi kabichi na maharage, au mchicha
Usisahau kukaribisha fisi
 
USA wanatoa 100$ kwa kila mpimwaji[emoji16][emoji16][emoji16]

Hapa ndio wanazidi kutuvuruga sasa na hizi chanjo.
Tanzania kila mhudumu wa afya atakaye shiriki kwenye kuchanja atapewa 2,000,000!Kwa hali hii ni mjinga tu atakaye-kubali kuchanjwa!
 
Nashauri kwenye pilau watumie Mchele wa Kyela. Wali maji watumie Mchele wa IFAKARA! Nyama sio lazima, sie wengine Marastafari. Maharage yanatosha
 
Back
Top Bottom