#COVID19 Nashauri Serikali wapike pilau na nyama pia na soda kwenye vituo vya kutolea chanjo


Mzee wa ubwabwa Hashim Rungwe Sipunda kushiriki. Atafanikisha hili.
🤣🤣🤣
 
Pilau litaliwa na chanjo wasichanje hata mmoja, hivi unawajua wabongo vizuri lakini?
Kuna wengine kwenye mazishi wanakula pilau la Marehemu na bado hawaendi kumzika Marehemu, ndiyo maana siku hizi kuna familia zinazofiwa hua zinaomba watu wakazike kwanza alafu ndiyo warudi Nyumbani kwa Marehemu wapate sunaa!! Kisingizio watakuambia watu wajikoni ndiyo wamezinguwa hadi Msosi ukachelewa!!
 
Kizuri kinajiuza wewe lofa, acha ujinga. Hivi mnadhani Watanzania ni wajinga kihivyo? Sasa hiyo si bait, wanaona!
 


We umewaona Wabongo ni waroho??
 
Pilau litaliwa na chanjo wasichanje hata mmoja, hivi unawajua wabongo vizuri lakini?
Ukimaliza kuchanjwa ndiyo unapewa mlo. Maelezo iwe kwa sababu wengine wakishachanjwa wanaweza kukosa nguvu, ndiyo maana baada ya kuchanjwa unapewa chakula.

Aliyeleta hili wazo lazima atakuwa ni think tank ya CCM. Mbinu hii wanaitumia sana CCM kwenye uchaguzi.
 
Pilau na nyama ndo itakuwa sawa na ile dola 100 wanayolipa kule marekani kama fidia, siyo?
 
Wawalete na wasanii, kina Diamond!
 
Hii kazi wai out source kwa Hashim Rungwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…