Nashauri serikali za mataifa ya Afrika ziendelee na mipango ya kuwaondoa raia wake nchini Afrika Kusini, kinacho endelea kinatisha

Nashauri serikali za mataifa ya Afrika ziendelee na mipango ya kuwaondoa raia wake nchini Afrika Kusini, kinacho endelea kinatisha

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Kushambuliwa kwa raia wa kigeni jijini Durban, Afrika Kusini, na kundi la takribani watu 50 kunaibua maswali kuhusu usalama wa wahamiaji nchini humo, hasa katika kipindi ambacho kumekuwa na maandamano dhidi ya wahamiaji katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Kwa miaka kadhaa, suala la wahamiaji nchini Afrika Kusini limekuwa likiibua mijadala kuhusu ajira, hali ya uchumi, huduma za kijamii na ushindani wa fursa za kiuchumi.

Baadhi ya wananchi wamekuwa wakielekeza lawama kwa wahamiaji wakihusisha uwepo wao na changamoto hizo, hali ambayo wakati mwingine imeambatana na maandamano na mashambulizi dhidi ya watu wanaodhaniwa kuwa wageni.

Kwa mtazamo huo, nashauri mataifa ya Afrika kuimarisha juhudi za kuwalinda raia wake wanaoishi Afrika Kusini. Serikali zinapaswa kufuatilia kwa karibu hali ya usalama, kutoa tahadhari za safari, kuweka wazi njia za kupata msaada wa kibalozi na kuandaa mipango ya dharura ya kuwahamisha raia walio katika maeneo yenye hatari kubwa inapohitajika.



 
Pole sana ndugu zetu wa afrika kwa madhila ambayo mnapitia wakati huu, rai yangu kwa mamlaka husika zitafute suluhu ya kuwaondoa wageni kistaarabu na wawaruhusu wauze basi hata mali zao walizochuma nchini humo na sio kuwaondoa mikono mitupu wawe na utu je, wakirejea kwenye mataifa yao wataanzia wapi kama mnawapora mali zao.
 
Hao watu si warejee makwao kwani huko walikotoka waliua watu!!!???

Ngoja waje wauliwe tu shauri zao.
 
Back
Top Bottom