Lodrick Thomas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2017
- 1,339
- 2,431
Moja kati ya timu za mpira nnazozikubai ni timu ya soka ya ujerumani!!Hawa wachezaji wanaocheza ligi mbalimbali wanatuangusha miaka nenda rudi. Na tatizo kubwa utasikia nichemistry. Kwamba hawajazoeana. Nashauri tuwe na timu ya taifa kama waajiliwa rasmi. Kazi yao iwe ni kutoka asubuhi nyumbani kwenda kujifunza mpira na kufanya mazoezi na kucheza mechi za kirafiki. Siku ya mechi wanatumika hao waliozoeana kila siku. Kipindi cha usajili timu ya taifa nayo iwe inagombaniana na vilabu kwenye usajili. Tunaweza kuwa na timu bora kwa mtindo huu.
Mfumo wa kuchukua wachezaji wanaocheA ligi unafanya kazu kwa wenzetu ila unaonekana kwetu umefeli.
Hawa watu wana malengo na fucus kubwa sana kwenye mpira!! yaani wana timu karibu tatu na zote zina uwezo wa kushindana na timu yoyote duniani!! angalia mashindano yaliyoisha juzi kati na ujerumani kuchukua kombe...kwenye kikosi hakuwepo muller wala ozili wala toni krooz lakini kombe walibeba!!
Mpira wa miguu bila malengo hatuwezi fika mahali, je tz tuna academy za mpira?? leo hii ukitaja timu ya taifa unajua kabisa akina ulimwengu ...samata lazima wawepo lakin kwa ujerumani mambo ni tofauti!!
Hatuwezi endelea kama hatuna msingi wa soka, soka lianzie chini kwa watoto hasa huko sekondari!! tuache siasa kwenye mpira!!