Nashauri uanzishwe mtandao wa simu wa kupiga na kupokea tu pamoja na sms. Watapiga hela mpaka wazikimbie

HOPEfull

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
1,882
Reaction score
2,313
Salamu.

Kwanza watawahamisha mazima wateja wote kutoka mitandao mingine na kuingia kwao kwa sababu watakuwa na vifurushi vyenye gharama nafuu hii itatokana na gharama za kuendesha mtandao zitakuwa ndogo kutokana na kutojihusisha na internet.

Internet inakula gharama sana kwenye matumizi na uendeshaji.Sisi wateja pamoja na haya makampuni ya mawasiliano tunakiona cha moto kwenye matumizi ya simu kutokana na gharama za internet.

Kuhudumia internet kunakula sana gharama kuanzia kwenye mitambo, kulipa mafundi, ufuatiliaji kuhakikisha mitambo ipo vizuri na network haikatiki gharama za usafiri nk.

Hi ni Siri yao lkn gharama za internet inaelekea zinawapekeka puta sana haya makampuni na ndio maana vifurushi vinapanda kila siku.Hii inasababisha sisi wateja kuumia.

Sijasema kusiwepo na makampuni yanayotoa huduma za internet,hapana kwa Sasa internet ndio kila kitu..bali nashauri ianzishwe kampuni ya simu itakayodeal na kupiga na kupokea tu pamoja na sms.

Pia sio lazima kuanzisha mtandao mwingine,hata hii iliyopo inaweza mmoja akaamua tu kuondoa deal la internet na kubaki kwenye 'call an receive na sms tu' Kwa sababu anakuwa tayari ana minara maeneo mengi kinachobaki hapo ni kufanya amendment tu.

Halafu wateja wengi wa simu hawatumii internet. Inawezekana robo tatu ya wateja wa makampuni haya mawasiliano ya simu hawatumii internet.Sina takwimu labda wenye takwimu watupe..ivo atawakomba wateja wengi sana kutokana na gharama zitakua poa na watakuwa na uwezo wa kuviremba vifurushi vyao wanavotaka tofauti na sasa ambapo kubadilisha vifurushi inakuwa ugomvi mkubwa sana.

Mitandao ya mawasiliano kazi kwenu msing'ang'anie kitu kimoja tu kinachofanana jaribuni kuwa tofauti kidogo sio lazima mfanane.🖐️
 
Mitandao ya mawasiliano kazi kwenu msing'ang'anie kitu kimoja tu kinachofanana jaribuni kuwa tofauti kidogo sio lazima mfanane.[emoji2772]
Dunia hairudi nyuma!zama zimepita hizo
 
Mbona sasa hivi gharama za kupiga ni karibu sawa au pungufu ya miaka 10 iliyopita!

Mwaka 2008 vodacom walikuwa na kifurushi kiliitwa chizika kwa bei ya 1,500. Hiki unapiga simu kuanzia saa 06:00 hadi saa 17:00 bure yaani kwa gharama ile ile ila ni kwa voda to voda

Leo mwaka 2023 ukiwa na 2000 unajipatia dakika 600 za kupiga wiki nzima kwa uhuru.

Kipi rahisi?
 
unamaanisha hiyo kampuni isijihusishe na miamala ya kifedha, bima, huduma za kibenki, malipo kwa njia ya simu, kuchezesha bahati nasibu, huduma nyinginezo nk... si ndiyo?
 
Wanaweza wakaona wapi wakaanglia kuona wapi kunalipa.Huduma hizo watumiao ni wachache Sana
 
Naona umezungumzia wanakula sana hasara mbona hujazungumzia namna gani wanavyokula faida.
 
Nadhani ungefanya kautafiti kidogo kujua ni huduma gani kati ya "data" na "voice" zinaingiza mapato makubwa kwa sasa ambapo makampuni yote yanatoa hizo huduma zote kwa pamoja. Alafu uje kujiuliza vipi yule atakaye fanya "voice" pekee ndio awe mauzo makubwa?
 
Mbona sasa hivi gharama za kupiga ni karibu sawa au pungufu ya miaka 10 iliyopita!

Mwaka 2008 vodacom walikuwa na kifurushi kiliitwa chizika kwa bei ya 1,500. Hiki unapiga simu kuanzia saa 06:00 hadi saa 17:00 bure yaani kwa gharama ile ile ila ni kwa voda to voda

Leo mwaka 2023 ukiwa na 2000 unajipatia dakika 600 za kupiga wiki nzima kwa uhuru.

Kipi rahisi?
Ukichanganya gharama za huduma zinazotolewa kama "promotion" badala ya kuangalia gharama halisi utapotea tuu. Ukitaka kujua gharama halisi hata sasa piga out of bundle alafu linganisha.
 
Nadhani ungefanya kautafiti kidogo kujua ni huduma gani kati ya "data" na "voice" zinaingiza mapato makubwa kwa sasa ambapo makampuni yote yanatoa hizo huduma zote kwa pamoja. Alafu uje kujiuliza vipi yule atakaye fanya "voice" pekee ndio awe mauzo makubwa?
Mimi kwa mtazamo wa nje naona gharama za internet zinawanyonya hata wale wasiotumia internet.Wasiotumia internet wanawasaidia wale wanaotumia katika gharama za uendeshaji.

internet inaonekana ina gharama sana ndio maana humu mitaani kuna visehemu binafsi vichache sana vinavotoa huduma hiyo.
 
Nitoe mfano shirika la posta lilishakua na huduma hii zamani wangefanya kuidumisha kisasa zaidi wangeachana na hayo mainternet na uzuri wana mitambo yao nchi nzima. wangefanya kuboresha tu.Yaani walikuwa wanateleza tu kwenye ganda la ndizi.
 
Hao wezi wengine watakubali maana wale wengine sijui kama wamepata kubali nilichoka miaka kadhaa nyuma walitaka tuwe nalipia video call za Nje yule Tura alikua Waziri baadae wakawaita WhatsApp waone ni jinsi gani wanaweza kukusanya Kodi WhatsApp waliwaambia kusanyeni kodi kwenye bando huko huku sisi hatuhitaji hizo mambo wakajifanya kuangalia kampuni ambayo itaweza kufanya huo Ujinga WhatsApp waliwaambia mkichezea mambo zetu tutaondoa kabisaa naona Kaizari katulia kimya...
 
Back
Top Bottom