Muhimu bunge likatunga kanuni kutofautisha muda wa kuchangia wabunge kulingana na sifa ya eiimu na makundi yanayotoka. Kwa mfano wenye elimu ya PhD wakawa na muda mrefu tofauti na wale darasa la saba, mbunge wa jimbo akawa na muda zaidi ya wale wa viti maalumu.
Hatusitahili kuchuka kila kitu kutoka kwa mataifa makubwa, wenzetu wana wabunge wenye taaluma na uelewa unaofanana. Wanajua kazi za mbunge na anatakiwa kuchangia nini juu ya wizara husika na anajua hiyo wizara inatekeleza nini. Kwa mfano mbunge anasimama na kuanza kuorodhesha miradi iliyotekelezwa na serikali katika jimbo lake. Serikali inaijua na wananchi jimboni kwake wanaiona, huo ni upotezaji wa muda wa kuwapa akina Dr. Kimei kuishauri serikali namna bora ya kutatua kuadimika Kwa dola nchini.
Wakati bunge lina Kambi Rasmi ya Upinzani, KUB alipewa upendeleo wa kila aina, atakuwa wa kwanza kuulizwa swali Kwa Waziri Mkuu, akisimama na mbunge mwenzake wa Upinzani ni lazima apewe nafasi yeye. Huu siyo ubaguzi. Wakati niko chuo kikuu tulitembelewa na Rais baada ya hotuba yake yalifuata maswali, wahadhiri walinyosha mikono wakati mhadhili mmoja aliyekuwa na kiwango kidogo alipoona na Profesa amenyosha mkono lakini ikiwa imebaki nafasi moja ya kuulizwa swali aliomba nafasi yake aulize yule Profesa, ambaye alikuwa hachagulwi. Hiyo ilikuwa kanuni waliyojiwekea wanataaluma. Hivi ni vigezo vya kawaida na isieleweke kama ubaguzi.
Hii ya kuwapa wabunge muda tofauti wa kutoa michango yao, itasaidia wale wenye uwezo mkubwa zaidi kuwa na muda wa kutosha kuishauri serikali. Nimesikia mchango wa Dr. Kimei na mbunge Babu Tale nilitamani muda wa Babu Tale upunguze na uhamishiwe Kwa Dr. Kimei.