Nashauri Watanzania tuanzishe utaratibu wa kuchoma moto maiti

Nashauri Watanzania tuanzishe utaratibu wa kuchoma moto maiti

Ndugu zangu Waislam someni huu uzi hii ya kuzika mtu mapema mnaweza kuzika watu walio hai wengi sana.

Na sio ajabu wanafufuka tena wakiwa kaburini halafu hufa kwa hofu na kukosa oxyjeni siajabu hupiga kelele sana mpaka wanakata roho....

Kwa sasa nimeanza kuogopa kuzikwa naona bora hi ya kuchoma moto

Kwangu Mimi kitu kibaya kuhusu kifo ni kaburi, haijalishi kuwa unaofukiwa pale ni mwili na si roho lakini lile shimo la futi sita sio kitu nnachotamani hata kidogo.

How did you feel ukijua ndugu yako uliyezika ameanza kuoza na kuoiwa na wadudu hii hupati hofu.

So bora kuchoma kujua tu hamna ishu tena going on kwa mpendwa wako

Bujibuji Simba Nyamaume

Aliwahi kusema

""Katika vitu nisivyovipenda ni pamoja na kutambikia mizimu. Nitafurahi sana na wabongo tukianza kuchoma maiti."""

Kwanini tusianze kuchoma tu wakuu...

Mfano mimi nikasema nitakapo kufa sitaki kuzikwa nataka kuchomwa na mkijaribu kunizika tarudi kama mzimu tawapelekea moto woote walioshiriki mazishi yangu kuaanzia wachimbaji mpaka ndugu zangu kina fundi bishoo

Hii itakaaje wakuu...?

Kaburi linatisha mjue.

View attachment 3073336

View attachment 3073337
Simple and clear
huoni kama n ukatlili tutakua tunakufanyia mkuu
 
Sisemi ishu ya kufufuka .
Mkuu kufa ni process mtu hafi gafula bin vuuu...

Sasa kujua kuwa mtu kakata moto mazima ni shughuli mana kuna kitu kinaitwa comma mkuu
Ukifa, moyo unasimama, pumzi inakata, joto linatoweka

Ukiingia kwenye comma, hivyo vyote unakuwa navyo ila tu fahamu ndo haifanyi kazi
 
Sisi waafrika sio tamaduni zetu hizo. Wao wanachomana ku-save ardhi na hawaamini tena dini. Ukizikwa kule wewe ni tajiri au mtu maarufu mwenye legacy fulani. Wanatunza kumbukumbu kwa vizazi vijavyo, ukiwa kapuku ni moto.

Mbali na kusema kwamba eti Afrika zamani mtu akifa familia inamtenga na kuhama... Ni kweli lakini sio pote, baadhi ya jamii walikuwa na akili ya kufukia miaka mingi tu iliyopita, ila baadae kukawa na utaratibu bora baada ya dini kuja.

Huku hilo swala haliwezi kupitishwa.
 
Sisi waafrika sio tamaduni zetu hizo. Wao wanachomana ku-save ardhi na hawaamini tena dini. Ukizikwa kule wewe ni tajiri au mtu maarufu mwenye legacy fulani. Wanatunza kumbukumbu kwa vizazi vijavyo, ukiwa kapuku ni moto.

Mbali na kusema kwamba eti Afrika zamani mtu akifa familia inamtenga na kuhama... Ni kweli lakini sio pote, baadhi ya jamii walikuwa na akili ya kufukia miaka mingi tu iliyopita, ila baadae kukawa na utaratibu bora baada ya dini kuja.

Huku hilo swala haliwezi kupitishwa.
Hili suala sasa ndo nataka lifanyike kwangu vipi ndgu wanaweza kataa au
 
Hili suala sasa ndo nataka lifanyike kwangu vipi ndgu wanaweza kataa au
Hakuna dini imeagiza maiti au Marhum achomwe... Ukiruhusu iwe against na watu wakafanya hivyo unakuwa umefanya kufuru mapema. Mwenyezi mungu hana radhi nawe

Moto ni adhabu, si sahihi wanadamu kutendeana hilo. Yeye pekee ndio atakayeadhibu kwa moto.

Natamani nikueleweshe zaidi... Ila muda na tayari imeshakuwa sikio la kufa
 
Sasa mkuu si bora moto kula kitu kinaisha pale pale .....

Hi ya kuzika ndo inapelekea watu kutambika makaburi...
Kifo ni kama usingizi.kila linalofanyika na watu unasikia ila hauwezi kujibu wala kufanya chochote.sasa uchungu wa kutolewa roho bado unao alafu wakuongezee na moto?
 
Nasikia kwenye uislamu kule kaburini unapata mateso sana kama ulikuwa muovu duniani, sasa je hawa wanaochomwa moto hizo adhabu za kaburi inakuwa wame cheat ama?
FaizaFoxy anaweza kuwa na jibu.
 
Utu uzima una mengi sana. Hata mawazo ya kufa kufa mnayatoaga wapi?
 
Mimi naona hilo wazo ni zuri Ila napendekeza haya

MTU akifa viungo vyake baadhi vivunwe ili visaidie walio hai

Maiti yake badala ya kuzikwa na kuchomwa wapewe wanyama wa porini wanaokula mizoga wapate kitoweo.


NB Mimi naona huu utaratibu uendelee
 
Back
Top Bottom