Nashindwa kuelewa kama hii mimba mimi nahusika

Travis samwel

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2013
Posts
215
Reaction score
42
Mimi nna mpenzi wangu ambaye nipo nae kwa muda wa mwaka mmoja sasa, sasa hivi ananiambia kuwa ana mimba yangu. Yeye huwa anaingia period tar 17 na mimi nilikutana naye kimwil tar 14, je hapo kuna uwezekano wa mwanamke kupata mimba jamaniii?

Naomba msaaada wenu wadau ili niondoe huu utata!
 
Hiyo mimba ni yako acha kuleta zengwe na utashangaa mtoto atazaliwa anafanana na wewe mbaya mpaka utaona aibu. Mbegu za mwanaume zinaweza kukaa mpaka masaa 72 zikiwa hai baada ya kuzimwaga huko kwenye naniihii. Isitoshe hizo ndiyo siku zake hasa za kushika ujauzito maana ungechelewa siku 3 zaidi yai lake lingepevuka na kupasuka na mwisho ungeona damu/hedhi ila kwakuwa yai lilirutubishwa siku 3 kabla basi halikupasuka hence UJAUZITO WAKO and no hedhi.

Kama ulikwa na nguvu za kutosha siku hiyo yaani kama hukuwa umelewa, basi kuna uwezekano akatokea mtoto wa kiume (ingawa chance ni masaa kadhaa kabla hajaanza siku zake maana x huwa hazikawii kufa tofauti na y ambazo zinaweza kudumu mpaka masaa 72 (kama sijachanganya kati ya y na x)).

Usiku mwema.
 
Hahaha...
Huo mzigo ni wako mkuu anza maandalizi ya kulea ujauzito.
Halafu kuna jambo moja ninataka kukusahihisha, mwanamke huwa hana tarehe maalumu ya ku-ovulate( yaani yai kupevuka).
Ukitaka maelezo zaidi usisite kuuliza.
 

asnte mkuu kwa msaada wako
 
Wengine akikuona bahili sana anakutoa hela kwenye hiyo mambo anajua kabisa hakosi 100,000 kushuka chini.
 
Kwa maelezo hayo hiyo mimba siyo yako. Period tar 17 umefanya tar 14 siku tatu kabla ya kuaza siku zake, haiwezekan ili apate mimba kama mzunguko wake ni siku 28 ungefanya kati ya tar 29-2.
 
kuanzia siku aliyopata hedhi hesabu mpaka siku kumi hizo ni safe (kama anaenda 4days una 6days za kujivinjari), then danger ni kuanzia siku ya kumi na moja mpaka kumi na tano, ndani ya hizo siku ya 11 mpaka ya 15 kuna siku ambapo yai ndio litapevuka na mwanamke anakuwa na hamu sana ya ku-do. Baada ya hapo days zote zilizobaki ni safe mpaka hedhi. Then unahesabu tena kama hapo juu.


kama yeye anapata hedhi tar 17 na mme-do tar 14 according to my statement it was safe day. What matters muulize last hedhi alianza lini then count kama hapo juu utapata jibu.
 
Yani hiyo mimba sio yako kabisa hata kama mzunguko wake ni wa siku 31 au 28 sio kabisa kwa mizunguko yote hiyo hesabu kama nilivyokueleza utakuta hizo tar zinafall under safe days.
 
Yani hiyo mimba sio yako kabisa hata kama mzunguko wake ni wa siku 31 au 28 sio kabisa kwa mizunguko yote hiyo hesabu kama nilivyokueleza utakuta hizo tar zinafall under safe days.

hebu nieleweshe jamaniii!! Huyu aliingia period tar 17 akamalza tar 22 mwez wa kwanza, then mm nikaja ku do nae tar 14 ya mwez wa 2 baada ya hapo demu akanimbia ana mimba
 
Fadhili Paulo, umeniaibisha mwalimu wa biology!
 
wewen kwa akili yako ulifikiri ni ya nani...?
 
hebu nieleweshe jamaniii!! Huyu aliingia period tar 17 akamalza tar 22 mwez wa kwanza, then mm nikaja ku do nae tar 14 ya mwez wa 2 baada ya hapo demu akanimbia ana mimba
Kama mchumba wako siku zake huwa hazina mabadiliko ya mara kwa mara. Kwa maana ya kwamba mzunguko wake ni siku 28 through out, basi haiwezekani kwake kupata mimba siku hiyo. Maana ilikuwa almost ndiyo siku yake ya kuanza hedhi nyingine.

Lakini huwa kuna exceptions kwamba mabadiliko ya hali ya hewa huweza kubadilisha mzunguko wa mwanamke. Hapo incidence kama hizo hutokea. Cycle ya mwanamke haipo perfect siku zote. Mabadiliko ya vyakula au pengine hali ya afya huweza kuibadilisha cycle yake pia. Kwa hiyo bado kuna probability kwamba yawezekana mimba ni yako. Lakini tukiassume hakukuwa na mabadiliko yoyote, basi hiyo mimba haikuhusu.

Biologically yai la mwanamke hupevuka siku kumi na nne kabla ya kuanza hedhi nyingine. Na likishapevuka hukaa kwa kati ya masaa 24 hadi 36 na baada ya hapo linakufa. Ili kuepusha mimba tunashauliwa tusikutane na wapendwa wetu kuanzia siku ya kumi na moja tangu apate hedhi hadi siku ya kumi na saba. Hiyo pia ni kwa vile yai huweza kuwahi au kuchelewa, lakini pia mbegu za mwanaume zinaweza kuishi ukeni kwa kati ya siku mbili hadi tatu. Nafikiri nimekupa jibu la kukusaidia.
 
maelezo ya ome hapo juu ndo sahihi.....kama ni uchunguzi wako ufanye kupitia maelezo yake
 
HIYO NI MIMBA YAKO MKUU SIKU ZA HATARI NI SIKU TANO KABLA YA HEDHI,KUANZIA TRH 13 NI HATARI KWAKE ALAFU SPERM AU MBEGU ZINAKAA KWA MWANAMKE MUDA WA MASAA 72,SAWA NA SIKU 3 ZIKISUBIR YAI ENDAPO HALIJAWA TAYAR HUTOKA KWA NJIA YA MKOJ O au ZINABADILISHWA KUWA CHAKULA CHA MWILI HESABU TOKA TRH 14 HAD CKU TATU MBELE KAMA HUJAMSABABISHIA JANGA NTOTO WA MWENZIO!!!by jenias wa shule ya kata
 
Kwa hesabu ya haraka na kama maelezo yako ni ya kweli iyo mimba siyo yako coz tar 14 wassafe day
 
Nani alikuambia au ulisoma wapi kuwa SIKU ZA HATARI NI SIKU TANO KABLA YA HEDHI?
hakuna kitu kama hicho, may be kama unataka umbambike huyu jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…