Mara nyingi ninapendelea kuwa peke yangu, ninakumbula mno mambo na maeneo niliyowahi kutembelea zamani, marafiki wa zamani, maisha ya utoto na michezo yote. Naumia na hulia sana nikikumbuka, havikuwa vitu vibaya ila najikuta nalia tu!
Muda mwingine ninapokula chakula nafikiria wengi wanaolala njaa ikiwemo watoto wadogo, hulia sana na chakula hakipiti, najikuta naacha kula na kulala.
Sina chochote kinachoweza kunipa faraja na raha, nipo mpweke na sijui chanzo chake, napenda kuwahudumia wanyama, na kuwatunza. Nina huruma na wanyama mno.
Kuna muda ninapokuwa peke yangu najikuta nakumbuka matukio ya zamani sana na huishia kulia tu, hata sijui ni nini hiki kinanipata. Sipendi kuongea ongea, wala kuchangamana na watu, n.k.
Jamani nishaurini ninapitia kipindi kigumu!
NB: Nina miaka 24, nasoma.