Nashindwa kujielewa hii ni hali gani?

Nashindwa kujielewa hii ni hali gani?

Nimedandia gari kwa mbele ila nimeshakujibu nilidhani wewe ni Ke kumbee Me basi tafuta Ke ule K unauhitaji huo ndio maana uko mupweke ila mashine ipoo au haipooo sawa??
Kwa maana siku hizi sie tunakutana na milenda tu nanguvu hakuna
Labda huna mvuto, na ndio maana husimama kama mlenda, mwanamke akikuvutia vizuri yaani kugusa tu kitu hicho, ngangari yaani!
 
Mara nyingi ninapendelea kuwa peke yangu, ninakumbula mno mambo na maeneo niliyowahi kutembelea zamani, marafiki wa zamani, maisha ya utoto na michezo yote. Naumia na hulia sana nikikumbuka, havikuwa vitu vibaya ila najikuta nalia tu!

Muda mwingine ninapokula chakula nafikiria wengi wanaolala njaa ikiwemo watoto wadogo, hulia sana na chakula hakipiti, najikuta naacha kula na kulala.

Sina chochote kinachoweza kunipa faraja na raha, nipo mpweke na sijui chanzo chake, napenda kuwahudumia wanyama, na kuwatunza. Nina huruma na wanyama mno.

Kuna muda ninapokuwa peke yangu najikuta nakumbuka matukio ya zamani sana na huishia kulia tu, hata sijui ni nini hiki kinanipata. Sipendi kuongea ongea, wala kuchangamana na watu, n.k.

Jamani nishaurini ninapitia kipindi kigumu!

NB: Nina miaka 24, nasoma.
Hizi ni zile zile dalili mkuu wa jeshi la polisi alizosema mtu akitaka kujiua wahi kituoni ukaripoti ili aokolewe
 
Cha kwanza.
Panga kila kitu unachopaswa kukifanya ndani ya siku yako.
Kitu cha kwa kwanza ukiamka iwe ni kutandika kitanda.
Kitu cha pili ni kwenda mazoezi. Ukifanya ya kukimbia ni vizuri zaidi.
Kitu cha tatu ukirudi mazoezi oga.
Kitu cha nne kuwa na jarida, au kitabu cha dini usome walau kwa nusu saa.
Kufanya hayo yote itakubidi uamke mapema. Na ili uamke mapema usichelewe kulala.
Ukifanya hayo siku yako itaanza kwenda vyema. Ukiweza hayo. Nitakuongezea mengine
 
You are an empath

Google ujijue zaidi kama ni kwei au laah
 
Hii ni dalili ya kufa aisee,omba sana na shirikiana na jamii yako kuendesha maisha,hudhuria ibada,jiunge na vikundi vya jogging au kwaya (Kama ni mkristo) shiriki shughuli za kijamii kwa kujilazimisha utakaa sawa!
Ukibaki na hiyo hali kwa hakika tutakupoteza siku si nyingi...pole sana
Hizo ni dalili za kufa kama si hiyo una dhiki sana za maisha.
 
Jichanganye na marafiki mzee.. Kama haupo kwenye mahusiano vuta mtoto utulie nae... Yaani Weka ndani kabisa uishi nae

Magonjwa ya akili yapo mengi sana.... Utaanza kuonea huruma mpaka magogo ya miti yanayoshinda barabarani wakipigwa na jua
 
Nasoma, sasa nitaoaje kaka?
 
Hata mimi nilikuwa hivo,nimebadilika baada ya kuanza
20210821_174928.jpg
 
Mara nyingi ninapendelea kuwa peke yangu, ninakumbula mno mambo na maeneo niliyowahi kutembelea zamani, marafiki wa zamani, maisha ya utoto na michezo yote. Naumia na hulia sana nikikumbuka, havikuwa vitu vibaya ila najikuta nalia tu!

Muda mwingine ninapokula chakula nafikiria wengi wanaolala njaa ikiwemo watoto wadogo, hulia sana na chakula hakipiti, najikuta naacha kula na kulala.

Sina chochote kinachoweza kunipa faraja na raha, nipo mpweke na sijui chanzo chake, napenda kuwahudumia wanyama, na kuwatunza. Nina huruma na wanyama mno.

Kuna muda ninapokuwa peke yangu najikuta nakumbuka matukio ya zamani sana na huishia kulia tu, hata sijui ni nini hiki kinanipata. Sipendi kuongea ongea, wala kuchangamana na watu, n.k.

Jamani nishaurini ninapitia kipindi kigumu!

NB: Nina miaka 24, nasoma.
Waone watu wako wa kiroho. Soma kwa bidii upate uamuzi na maarifa ya kuwasaidia wasiojiweza.
 
Tatzo ni kukosa ajira pesa na kazi maana ukiwa zako bize na kazi huo mda wa kulia lia utautoa wapi ndugu yangu
 
unatatizo la kutaka huruma kwa watu, nilikua na mdogo wangu alitusumbua sana, yaan yeye alikua analia shuleni anawaomba msaada wamsaidie, kanisani wanachanga wanampa dogo!
.
.
nilivyokuja kusikia niliumia na kuudhika sana!
.
.
dogo tatizo la watu kulala njaa sio lako, Mungu anajua kwanini ipo hivyo, ukiweza wasaidie usipoweza kausha na si lazima uwape msaada hio ipo tuu, jichanganye na watu, anza kushabikia mpira na usitoke nje, toka nenda maeneo ya beach, tafuta marafiki wa kutembeleana na kutoka kutembea, tafuta mpenz ila hapa kwa mpenz chunguza mdada naekupenda maana inavyoonesha utakua down sana mdada akikukataa, kazana kwenye masomo yako kwa juhudi bila kuwaza kumbukumbu za zamani, na zaidi hii dunia hatifahamu ilianzaje na kwanini ipo hivi, kuwa positive daima!!!!
.
.
maisha haya hayapendi watu wenye kulia lia, wenye kutafuta huruma, inawahitaji watu wenye jeuri ya kuyaongoza maisha wanavyotaka!
 
Tafuta demu na jichanganye na watu hapo chuo.

kwanza we wa kike au kiume?
 
Back
Top Bottom