Nashindwa kumsamehe huyu mpenzi wangu

Sawa, kama alifanya surgical abortion na hakufanyiwa na mtu ambaye ni mtaalam anaweza akapata majeraha kwenye uterus ambapo itakuwa ni ngumu kwake kupata ujauzito tena. Na dalili zake zinaendana na anazopitia...
alienda hospitali ya wahindi pale Mwanza inaitwa hindu Mandal, na tokea amepewa hizo dawa za mwezi mzima tokea mwaka jana mwezi wa 11, mpaka leo hajawai kukosa period.

Changamoto ni kwangu hatia inanitafuna sana kwamba mama alieniulia mtoto huyohuyo nirudi tena kwake kumpelekea mahari na ninakumbuka nilimsihi sana asifanye hivyo.
 
Huyo binti unaweza kuishi nae vizuri kama atakubali mama yake asim manipulate. Ila kama mama yake akiendelea kum control sahau kuhusu furaha.
Kuhusu mahari wewe peleka tu lakini ukishaoa, hakikisha binti anakuwa mbali na mama yake
 
Lakini...hukua umemuoa.... na alikua chini ya wazazi. Sidhani kama unatakiwa umchukie mama mkwe...

Wewe msamehe huyu binti na muoe...

Maisha yenyewe yako wapi. Hata dini inatusihi tusamehe

Usifanye moyo wako kuwa mgumu.
 
Mama mkwe anaingilia uhusuano na hujamuoa, ukimuoa utaona mengi....kimbia
 
Ndiyo hormonal imbalance inaathiri afya ya uzazi.

Huyo usioe kwa maana hiyo ndoa haitadumu na hamtaishiwa misukosuko.
 
"wataungana wawe kitu kimoja na hakuna rangi utaacha kuona!"
Hichi ndicho kitaenda kutokea mbele ya safari sasa wewe kaza fuvu kaoe huyo mwanamke..
 
Binti umempenda lakini mama ake ni kichefuchefu, ukiamuoa jua ndoa yenu haitafika mbali maana binti atakuwa anapokea maelekezo yote toka kwa mama ake ambaye ameshaonesha negativity katika mahusiano yenu.
Amua moja ukae na binti na amfungie vioo mamaake au ukabiliane na changamoto atakazozizalisha mama. Mimi kama mimi ningemuacha huyo binti kwa kukubali wazo la mamaake na kuniulia mwanangu na incase akihitaji msaada ningekuwa namsaidia nikiwa mbali.
 
Muache endelea na maisha yako.
 
Hormones imbalance ipo, wakati mwingine mwanamke akibadilisha mazingira inatokea ( Sumbawanga kuna baridi)
Kuhusu mama wa binti kweli ni tatizo, ila usimuhukumu binti kwa kuzaliwa na mama wa hovyo.
Kikubwa mmeshajua wote kuwa huyo mama ni tatizo na mpange mkakati wa kumthibiti.
Hautapata mwanamke perfect, ukimwacha huyo sababu ya mama yake unaweza kupata mwingine ambaye anashinda nyingine mbaya zaidi.
 
Mtoto wa kike na mama yake lao Moja...baada ya kulitambua Hilo huyo mama angeamua kukushtaki kuwa umekula mwanafunzi ungesweka 30yrs ndichi,so mshukuru,ila kupenda hela,hakuna ma mkwe asiyependa maokoto jikaze weka chombo ndani.
 
Msamehe, weka ndani mutoto mzuri huyo...

Jifunze kupambana na changamoto na siyo kukimbia...
 
ushautua huo mzigo wa misumari kwa gharama ya 400,000/= kwanini unataka kuurudisha na viashiria vyote vya hatari ushaviona? tumia akili usitumie hisia.
 
Hivi ujasili wa kumuita mama mkwe unautoa wapi na hujamuoa binti yake?? Kwahiyo ulitaka akuchekee unavyomuharibu binti yake??!!
Kazi unayo lakini kwenda kwao kujitambulisha hutaki, unataka kuweka mimba mxieeeewwww
 
Kama serikali inaajiri watu kama hawa, bas halali tusiendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…