Nashindwa kumsamehe Magufuli kwa hili

Lakini MUNGU wetu wa mbinguni alishughulika naye vizuri sn hatakaa asahau
 
Msamehe,usiposamehe wewe pia hutasamehewa,lakini pia hakuna ushahidi kuwa magu ndio alimpiga risasi lisu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Umenielewa vibaya sikusema alimpiga risasi Lisuu ila km mkuu wa nchi kukaa kimya kwa tukio km lile kwa mtu ambae alikua mkosoaji wake mkuu ilikua inamaanisha nn

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Upo kama mm mkuu, kwa nchi za wenzetu zenye kufuata sheria na taratibu, mwamba ilibidi ang'atuke na awe nyuma ya nondo saa hzi kwa kushindwa kulinda raia na mali zao kama alivyoapa. Mbaya zaid alikaa kimya kabisa as if hajui ni kitu gan kimetokea. Mungu amuhifadhi panapostahili.
 
wanasema msamaha sio kwa ajiri ya unayempa,ni kwa ajiri yako mwenyewe.

1.katika hili huna ushahidi wa moja kwa moja kwamba alihusika au laah,unajipa mzigo mziti kuubeba.
2.hhapungukiwi na chochote,unajipa umuhimu usiokuwa nao.

3.hakuna aliyekuuliza au kukuomba umsamehe,unajipa umuhimu usiokuwa nao pia.

kama hutasamehe kwa faida yako,ni chuki yako inatakayokuua mwenyewe,maana kila sehemu anasifiwa tu.
 
Wakati wa utawala wa Magufuli Watu walikuwa wanawindwa kama Digidigi.
Waliokuwa wanawinda wenzao kisasi kinawahusu. Yale mambo ya mara umemtukana rais sijui wewe msaliti ooh unahujumu au unashirikiana na mabeberu.

Lazima walipwe haki Yao. Maana jiwe hayupo tena.

Angalia picture ya sabaya akiwa msibani kwa magufuli alikuwa analia as if magufuli alikuwa baba yake. Kumbe walikuwa na mambo Yao.

Nchi ilikuwa inaelekea kubaya sana
 
Mimi ni lile la Alphonce Mawazo, kucharangwa mashoka & mapanga na vijana wanaojulikana (wasiojulikana) mchana kweupe.

Mbaya zaidi askari wetu waliwafuata waombolezaji hospital Bugando kwenda kuwapiga mabomu ya machozi mochwari. Ili tu Mawazo asiombolezwe wala kusindikizwa kwa heshima. Mpaka mahakama iliporuhusu aagwe!!. Nilijiuliza ni nini anachokitaka bwana mkubwa ?!.

Kilichoudhi so called uvccm kwenda kuvuruga na kufukua kaburi lake . Mungu ni fundi tena stadi. [emoji24][emoji879]
 
Mimi ninatamani niende na Bulldozer kwenye kaburi lake nikatifuetifue kwa mambo aliyonifanyia wakati wa Uchaguzi mkuu wa 2020.
 
Aibu huoni?
 
Allijua kuwa mchezo ule ni wa mbowe so acha wafu wazikane.
 
Watu wanashindwa kufahamu siasa inamichezo mingi michafu!.
Inanipa wakati mgumu kwa namna tukio lile lilivyotokea kuwa kulikuwa na nguvu ya rais!!. Tukio lilifanyika kicholeshaji sana na kigaidi mno watu hufikiri upande mmoja wa kuwa rais anahusika hawafikiri rais pia huwa anamaadui na wanaweza kuchoresha tukio kama lile ili kuharibu taswira yake!.

Vitu haviendi vile wengi wanavyoona picha huchoreshwa..
Matukio kama haya hata kwenye nchi kubwa huleta utata just nchi Kama marekani bado hawajatolea ufafanuzi wa kina juu ya kifo cha aliekuwa rais wao jf Kennedy!. Zigo Kama hilo hukuta serikali iliyofuata ndio hutupiwa.

Nafikiri vitu Kama hivi huvikalia kimya kwamaana huona ukimya unastahili kwa wakati huo,muda wa sisi kuja kutoa hukumu utafika taarifa sahihi zitakapotolewa tuacheni ramli.
 
Sawa mkuu lakini mbona mkuu hakuonesha kuguswa hata kidogo, fikiria Mama Samia juzi alisemea kuhusu clip ya Askari aliekua anaisifia gongo na yule Askari amefukuzwa kazi vp kwa tukio km lile akikaa kimya nn maana yake

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Adhabu aliyopewa Magufuli na Mungu inamtosha, tushukuru kwa kuwa Lissu bado ni mzima pamoja na kwamba ushahidi wote wa mazingira unaonyesha kuwa mtuhumiwa Namba moja ni Magufuli.
 
Matukio yote ya kumshambulia binadamu sio mazuri hata kidogo.
Binadamu wanaroho ngumu sana na hawajali maisha ya watu wengine ndio maana kilasiku tuna sikia watu wanashambuliwa na kuuwawa kinyama.

Matukio kama hayo yalikuwepo kabla ya Magu, wakati wa Magu, na hata baada ya Magu tunasikia watu wanashambuliwa na kuuwawa kinyama, mengine ni juzi tu huko arusha tofauti ni aina tu ya mashambulizi lakini shambulizi ni shambulizitu.

Sasa wewe kama unaumia roho kiasihicho kwa sababu unahisi kwamba huyo usietaka kumsamehe ndio amehusika basi utakufa kwa kihoro.

Tunaambiwa hakuna dhambi ndogo,wewe kumbuka kuomba msamaha kwa uliowakosea ili upate rehema kwa Mungu wako, kutangazia watu kwamba hutamsamehe mtu fulani niujinga na upumbavu maana Mungu anataka watu kusameheana.
 
Samia alienda kumuona lissu alimpa pia salamu za rais..
Mkuu mbona huhoji hata uongozi uliopo sasa bado umekaa kimya kuhusu tukio hilo..?
Mkuu Kama utakuwa umenielewa vyema swali lako nishalijibu Soma komenti yangu ya Kwanza.
 
Kitendo cha kusema tunajenga kwa fedha zetu, wakati anakopa, deni la taifa kupaa, sijui alikuwa na maana gani! Kwani huko nyuma tulikuwa hatukopi? Kwahiyo ukikopa unasema unatumia fedha za ndani? Tofauti sasa iko wapi? Unatuambia tutembee vifua mbele, yaani sie macrazy? Usameeki Magu, na walio kuzunguka ambao uliwaweka karibu, polepole, bashiru, makonda, sabaya, ndugai, wote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…