Nashindwa kumsamehe Magufuli kwa hili

Nashindwa kumsamehe Magufuli kwa hili

Umenielewa tofauti ndugu! Hakuna niliposema jamaa alihusika au hakuhusika isipokuwa Jambo hili litazamwe kwa upana na sio kuelekea upande mmoja.
Ungelitazama kwa upana ungeanza na malalamiko aliyotoa Lissu kwa serikali kwamba kuna watu na gari zinamfuatilia wiki chache kabla hajapigwa risasi. Wewe unalitazama jambo hili kwa upana wa kimataga zaidi wala sio mtazamo huru.
 
Yule jamaa alikua mnafiki,Muongo grade 1.

Sikuwahi kumuamini hata mara moja kwa kauli zake baada ya kuona matendo yake...

Anaongea na mahisia yake kuwadanganya wenzie!

Mtu anafuata Kanuni za “Power “ bila kujua kuwa he is also a human being and he will die!

Njia nzuri ya kumtesa adui wako wa kisiasa siyo Kuua asee! Hasira huisha then nini hufuta kama Siyo majuto... You can teach people hata kupitia kesi ambayo hajui atatoka au la sometimes adi anafungwa then unakuja muachia

Unamkamata unampa onyo au anafungwa asijue atatok lini lakini siyo Kuua binadamu mwenzio!

Hata kumtesa binadamu mwenzio akatoka manundu siyo ubinadamu ni unyama na kutostaarabika

Nina wasiwasi kam huyu jamaa ataiona mbingu asee hata kam sijui eti alifanya kitubio sijui nini ila duu amekufa na majuto...


Watu wenye Roho mbaya vile ni kam wachawi na Huhangaika Sana hadi waje kuikata roho, wengine hadi Hunya ndipo wafe!

Ewe Mkuu yeyote usisahau kuwa na wewe ni Mtu/ Binadamu kama mwengine yeyote Mtu.

Kuua Binadamu mwenzio ni kujifanya wewe Siyo binadamu ni Zaidi yao kumbe wapi...
Ili kuepusha madaraka kuwapanda kichwani na kujiona Miungu, wafalme wa Dola ya Rumi walikua wanaajili mtu ambaye kazi yake ilikua kumkumbusha Mfalme kuwa ni binadamu na atakufa..

Mtumishi huyo alikua anatamka maneno “ you’re Mortal Cesar , You are Mortal Cesar, You are Mortal cesar “ hasa mfalme anapokua ameshinda vita au amefanya jambo la kishujaa”

Mfalme anae jua kuwa ipo siku atakufa humuepusha na kufanya mambo ya kipumbavu kama mengi aliyoyafanya Bwana Yule...

Usiue,Usiue!
Cc babukijana
 
Unaandika kishabiki sana hadi umeingia kwenye kichaka cha cha conspiracies za JFK kumtetea mpendwa wako. Ulichofanya ni kulinganisha machungwa na mananasi tu.

Ukiachilia mbali mtu aliyehusika na mauji ya Kennedy alijulikana na alikamatwa pia fahamu kwamba FBI na CIA walikwisha toa taarifa na wameendelea ku declassify ripoti nyingi kuhusu tukio zima la kuuwawa kwa JFK, kulikuwa hadi na kamati za seneti/bunge(live) na kamati maalum ya Rais kufuatilia, kujadili na kutoa repoti kuhusu tukio hilo.

Watu kuamini au kutaka kutokuamini majibu yaliyofanana ya FBI, CIA, kamati ya bunge na kamati ya Rais ni jambo lingine lakini angalau uchunguzi ulifanyika na taarifa ambazo hazipingani zilitolewa na vyombo vinne tofauti.Familia ya Kennedy na Chama chake cha Democrat hawana malalamiko au dukuku kuhusu kifo chake. Kwa upande mwingine hakujawahi kuwa na taarifa YOYOTE kwa taifa kutoka serikalini au bungeni kuhusu kushambuliwa kwa Lissu.
Haha! Mkuu fatilia kile kisa vizuri hadi kwanini alipewa gari lile la wazi nawakati haikupangwa.. muuwaji ndio alidabwa na ikiwa bado haujathibitika kuwa ni yeye kimahakama aliuliwa kwa kupigwa risasi hadharani!.. fatilia pia kwanini Trump alitaka documents za kifo cha Kennedy alitaka ziwekwe hadharani na wakati wameshatoa kila kitu..😄
 
Kila binadamu yoyote mwenye roho wa Mungu ndani yake ataumizwa na tukio lile, na ikitokea kama kuna aliyefurahi basi huyo ana roho wa shetani!

Ni kweli, sababu pekee ya kutofanyika jambo lolote ni kwasababu tukio hilo limeshuhudiwa live na mashuhuda wawili muhimu, ambao mpaka sasa, wamegoma kata kata kutoa ushirikiano kwa vyombo vya uchunguzi.https://www.jamiiforums.com/threads/shambulizi-la-lissu-wanaomdhania-dereva-anahusika-sio-wajinga-wana-hoja-za-msingi-je-anahusika.1479154/

Kama huu ndio msingi wa wewe kutomsamehe Magufuli, nakushauri tafuta nauli, kama huna, kopa, nenda Chato, kwenye kaburi lake, upige magoti, umuombe msamaha!.
Baada ya shambulio lile, Rais JPM, hakukaa kimya!.


Kwa vile hakukaa kimya, nakushauri nenda kamuombe msamaha marehemu!.
Kumsingizia marehemu kuna karma mbaya!.

Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana ambao mpaka leo hawajajulikana.

Nakushauri usihukumu usije ukahukumiwa! Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!.
P
Hivi kwa nini wabunge wa CCM na wana CCM wengine hawakwenda kumuona Nairobi? Kwa nini alizuiwa matibabu ya serikali? Kwa nini alinyimwa haki zake za kibunge?
 
Ungelitazama kwa upana ungeanza na malalamiko aliyotoa Lissu kwa serikali kwamba kuna watu na gari zinamfuatilia wiki chache kabla hajapigwa risasi. Wewe unalitazama jambo hili kwa upana wa kimataga zaidi wala sio mtazamo huru.
Okay mkuu mtazamo wangu ni kuwa sijui nani anahusika na tukio hilo la lissu unaweza nithibitishia kuwa unaemsema kuwa ndio mhusika..??
 
Dikteta Mzilakende alikua mtu katili sana.
Tumshukuru MUNGU alimwondoa kabla hajaleta madhara zaidi.
 
Bila ya kuwasahau Ben Saanane(alikua mmoja wetu humu ndani),viroba vya maiti pale COCO beach,Azory(gazeti lake la Mwananchi limemsahau)etc etc nikikumbuka haya ,hasira za kuuchukia utawala wa President Magufuri inachemka mno mwilini mwangu.
Hv ulitaka rais aende kufungua kesi ya Lissu kupigwa risasi wakti , mhusika na watu wake wa karibu hawakutaka kuonesha ushirikino kwa serikali , pia ni watu wabgapi wamepotea nchini hapa je wote kawapoteza Magufuri ? yaan kila anaepotea au kufa Chadema basi ni Magufuri ? ina maana kabla ya Magu , wanachama wa Chadema hawakuwai kukutwa na dhahama yyte ? Kuhusu maiti unajisahalisha swala la kibiti , unahisi serikali iliwaondoa wale jamaa kwa kuwaimbia ngonjera ? kuna muda waafrika tupunguze kuishi kwa uvumi bali tujitahidi kuongea mambo tuliyo na ushahidi nayo na si mtu kajisikia kumshutumu fulani basi ndo tunalibeba kama lilivyo na kuanza kulitumia mtaji kwenye siasa zetu , by the way mm sio ccm ila kuna vitu ukiniambia naona kama unanidharau Lissu kapigwa risasi tunamnyooshea Magufuri kidole ( kwa ushaidi upi ? Analalamika kutofanywa uchunguz , tutafanyaj uchunguz wkt hata muhanga wa tukio hataki ushirikiano na chombo husika ) WAAFRIKA TUNATUMIKA KIMCHONGO KUSHIBISHA MATUMBO YA WATU WACHACHE ndio maana walevi wa uchadema , uccm au u act huwa nawaona wapumbav tu stori zao nyingi ni za kusadikika na mihemko bila kujali usalama wa raia wema wasiojihusisha na siasa chafu na ukiwaomba ushaidi wengi wao wanaishia kukujibu vibaya maana hawana ushaidi wa wakiongeacho , Yangu ni hayo Muraa , tushikamane tulijenge Taifa. UCCM na UCHADEMA HAUTOTULISHIA WATOTO ZETU
 
Watu wanashindwa kufahamu siasa inamichezo mingi michafu!.
Inanipa wakati mgumu kwa namna tukio lile lilivyotokea kuwa kulikuwa na nguvu ya rais!!. Tukio lilifanyika kicholeshaji sana na kigaidi mno watu hufikiri upande mmoja wa kuwa rais anahusika hawafikiri rais pia huwa anamaadui na wanaweza kuchoresha tukio kama lile ili kuharibu taswira yake!.

Vitu haviendi vile wengi wanavyoona picha huchoreshwa..
Matukio kama haya hata kwenye nchi kubwa huleta utata just nchi Kama marekani bado hawajatolea ufafanuzi wa kina juu ya kifo cha aliekuwa rais wao jf Kennedy!. Zigo Kama hilo hukuta serikali iliyofuata ndio hutupiwa.

Nafikiri vitu Kama hivi huvikalia kimya kwamaana huona ukimya unastahili kwa wakati huo,muda wa sisi kuja kutoa hukumu utafika taarifa sahihi zitakapotolewa tuacheni ramli.
Kulikua na haja yoyote kuwazuia wabunge wa CCM na wanachama wengine wa CCM kwenda kumuona Lissu Nairobi? Kumnyima matibabu ya serikali? Kumnyima haki zake za kibunge?

Baada ya tukio lile tungeona jitihada za serikali kuhakikisha Lissu anakua hai na ushirikiano wa wabunge wenzake, isingeleta maswali sana. Mtu alijaa hasira hadi akawazuia watu wengine wasijihusishe na Lissu.

Katibu mkuu wizara ya afya aliyejihusisha kutoa matibabu ya awali pale Dodoma hospital alipelekwa kuwa balozi.
 
Okay mkuu mtazamo wangu ni kuwa sijui nani anahusika na tukio hilo la lissu unaweza nithibitishia kuwa unaemsema kuwa ndio mhusika..??
Haez kukupa ushaid wwte ni mihemko ndo inamsumbua , mf mm sio ccm ila hiko sio kigezo cha kukubali kila baya la ccm bila ushahidi , Siasa siyo Vita
 
Kitendo cha Magufuli Rais wa nchi Amiri jeshi mkuu mfariji mkuu kukaa kimya bila kujitokeza hadharani na kukemea lile tukio liliniumiza mno kwa nature ya Magu aliwezaje kukaa kimya what was behind the scenes
Wewe ni moja ya wahuni. Na sisi tumekubaliana ku #kataawahuni wote.

Screenshot_20211231-094831_Chrome.jpg
 
Yani ilionyesha kwamba anaweza kuuliwa mtu mda wowote na mahala popote Kwa utawala ule wa kishetani,hivi unaweza kupanua njia balabala nusu kilometer unawaambia watu walijenga kwenye hifadhi! Kule mwanza akasema hawa walipwe niwapiga kula wangu! Sina jema lakumkumbuka zaidi ya mateso Kwa binadamu wenzio
 
Haha! Mkuu fatilia kile kisa vizuri hadi kwanini alipewa gari lile la wazi nawakati haikupangwa.. muuwaji ndio alidabwa na ikiwa bado haujathibitika kuwa ni yeye kimahakama aliuliwa kwa kupigwa risasi hadharani!.. fatilia pia kwanini Trump alitaka documents za kifo cha Kennedy alitaka ziwekwe hadharani na wakati wameshatoa kila kitu..[emoji1]
Nje ya ripoti 4 rasmi conspiracies za kuwawa JFK zipo nyingi, hakuna kisa(conspiracy) kimoja tu, ziko nyingi, sijui unaniambia nifuatilie kisa kipi!. Hizi ni baadhi yake tu ; Mafia wa Chicago walimua baada ya kuwagekua, CIA walihusika, Israel, Cuba, Russia n.k wote wanatajwa kwenye mamia ya consiparicies zilizozagaa. Ni juu yako kuamini ripoti rasmi ambazo zipo au kuamini mmojawapo ya consipiracy unayoipenda na inayokuingia akilini, ila familia yake na chama chake cha Democrat hawakuwahi kutoka hadharani kutilia shaka hizo ripoti au kuonyesha kutoridhishwa, hiyo ni tofauti kabisa na suala la Lissu.
 
Back
Top Bottom