Nashindwa kumuelewa mume wangu, nikimkosea anaishia kulia

Nashindwa kumuelewa mume wangu, nikimkosea anaishia kulia

Nailaswrty

Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
20
Reaction score
30
Mimi na mume wangu tuna miezi minne sasa lakini mimi nimekua nikimkosea sana wala hanipigi anaishia kulia tuu na baadaye kuniambia kanisamehe.

Juzi amekuta nimechat na mwanaume kimapenzi ameniangalia tu akaanza kulia na kuniambia wala sijamkosea chochote niwe na amani kisha kesho yake anaamka akiwa normal kama hamna kitu nimemfanyia.

Jamani mimi nashindwa kumuelewa naombeni msaada wenu.[emoji24][emoji24]

1624869753438.png

 
Mvua zishapita na magunia ya mkaa bei imeshuka shauri yako.
 
Ndio maana!

Sasa wewe badala ya kumsaidia kwa Hilo tatizo alilonalo, wewe unamuongezea maumivu ya kuruka na wanaume wengine.

Huyo unazidi kumharibu zaidi kisaikolojia kwa kutoka na wanaume wengine. Suluhisho, mvumilie, mpe ushirikiano n.k, with time atakuwa sawa. Lakini ukiendelea hivi, unaweza kukuta amejidhuru au kukudhuru wewe!

Karibu Tena!
 
Wanawake ni pasua kichwa.
Kwaio ulitaka akudunde mi ngumi upoteze fahamu,ukiznduka unasema kweli nimepigwa na ungeposti majeraha hp jf na kwingneko,ukisema ukandamizaji.

Umeachwa hujapigwa,Mtoto wa watu hajazoea vita na kupigana.
Wewe unakuja ku post humuelewi.
Aisee wanawake hawajui wanachokitafuta kabisa.
 
Back
Top Bottom