"Nashindwa kupumua" ni sauti ya Afrika kwa ujumla, George Floyd ni sampuli

Mwenye nguvu wanaungana kumkabili mnyonge, mwendo wa goti tu, hapo tutapumuaje!!.
 
Kwa uchungu sana naandika " I can't breath". Kauli hii ni kumbukumbu ya madhila ya ubaguzi na unyanyasaji wa utu wa watu weusi unaofanywa Wazungu "weupe".

George Floyd ametamka sentensi ya mwishonimwishoni kwa ufasaha licha ya kuwa chini ya mgandamizo mkubwa wa goti la polisi mweupe.Namchukulia George Floyd kama sauti ya uwakilishi wa Mama Afrika.

Afrika inasema " I can't breath"kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni n.k imewekewa goti shingoni haiwezi kupumua vizuri na bado inazidi kugandamizwa zaidi.

Tunashuhudia Nchi kadhaa katika Afrika zikiwa katika hali mbaya ya kushindwa kupumua kutokana na vita vya kutengeneza, maradhi n.k vyenye chanzo chake kwenye maslahi ya mtu mweupe.

Masuala ya Afrika na ya Nchi mojamoja yanaingiliwa kwa kiasi kikubwa na maslahi ya mtu mweupe kiasi cha kupotosha kila jambo litakalowafanya wazawa waone faida halisi na matunda halisi ya jitihada zao.

Afrika inashindwa kupumua hata kwenye masuala ua uzazi wa mpango. Tumeshaambiwa kiwango cha ongezeko la idadi ya watu weusi ni kikubwa hivyo kuna haja ya kupanga uzazi na siyo kujipangia uzazi.

Afrika haipumui kwenye viwanda kwa sababu viwanda vyake ni kuchanga na vinashindanishwa na viwanda vyenye miaka zaidi ya 200 tangu kuanzisha kwake "sheria ya msituni".

Afrika inataka kuoneshwa kuwa haina maarifa yake ya asili " indigenous knowledge" na badala yake tunaona ikikosolewa na kuonekana kama inakosea inapotaka kutumia maarifa yake rejea dawa ya "Covid organics" ilivyopata upinzani kama kwamba Afrika haikuwa na dawa zake za aina yoyote na inapaswa kusubiri zinazoandaliwa na watu weupe.

Makanisani Afrika inafundishwa utamaduni mwingine kabisa leo hakuna ngoma,hakuna marimba, hakuna matari hakuna asili yoyote ya Africa Kanisani kwani tunaimba kizungu, tunasali kizungu tunaabudu kizungu jambo linalofanya uasili wetu kushindwa kupumua.

Pumzika George umetuwakilisha vizuri kwenye safari yako. Hatupumui vizuri ila tunapambania uhai bado chini ya goti la mkandamizaji.
"Siwezi kupumua" tafsiri yako sio rasmi.
Kama ndio nukuu toka usa basi ingesomeka NASHINDWA KUPUMUA.
 
Afrika itubu kwanza dhambi ya ubaguzi iliyopo ndani ya Afrika,kisha wapige kelele ya ubaguzi kwa watu wengine,zima kwanza moto uliopo katika nyumba yako,kisha nenda kazime kwa jirani,dhambi ya ubaguzi bado ipo katika damu ya muafrika mwenyewe.
We Afrika umebaguliwa nani mbona unafikra za kitumwa sana
 
"Siwezi kupumua" tafsiri yako sio rasmi.
Kama ndio nukuu toka usa basi ingesomeka NASHINDWA KUPUMUA.
Asante kwa ufafanuzi mzuri zaidi ila maana yangu nadhani imeeleweka
 
Kwa maoni Yangu wale waliokua wanashuhudia ilibidi waaingilie kati kwa namna yoyote ile
... tafsiri yake ingekuwa kumzuia afisa wa polisi kutekeleza majukumu yake na angekuwa na haki kisheria ya kuwapiga risasi kujilinda. Walitumia akili sana otherwise wangekufa wengi pale huku sheria ikimlinda yule polisi.
 
Naam
 
Kwa uchungu sana naandika " I can't breath". Kauli hii ni kumbukumbu ya madhila ya ubaguzi na unyanyasaji wa utu wa watu weusi unaofanywa Wazungu "weupe".

George Floyd ametamka sentensi ya mwishonimwishoni kwa ufasaha licha ya kuwa chini ya mgandamizo mkubwa wa goti la polisi mweupe.Namchukulia George Floyd kama sauti ya uwakilishi wa Mama Afrika.

Afrika inasema " I can't breath"kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni n.k imewekewa goti shingoni haiwezi kupumua vizuri na bado inazidi kugandamizwa zaidi.

Tunashuhudia Nchi kadhaa katika Afrika zikiwa katika hali mbaya ya kushindwa kupumua kutokana na vita vya kutengeneza, maradhi n.k vyenye chanzo chake kwenye maslahi ya mtu mweupe.

Masuala ya Afrika na ya Nchi mojamoja yanaingiliwa kwa kiasi kikubwa na maslahi ya mtu mweupe kiasi cha kupotosha kila jambo litakalowafanya wazawa waone faida halisi na matunda halisi ya jitihada zao.

Afrika inashindwa kupumua hata kwenye masuala ua uzazi wa mpango. Tumeshaambiwa kiwango cha ongezeko la idadi ya watu weusi ni kikubwa hivyo kuna haja ya kupanga uzazi na siyo kujipangia uzazi.

Afrika haipumui kwenye viwanda kwa sababu viwanda vyake ni kuchanga na vinashindanishwa na viwanda vyenye miaka zaidi ya 200 tangu kuanzisha kwake "sheria ya msituni".

Afrika inataka kuoneshwa kuwa haina maarifa yake ya asili " indigenous knowledge" na badala yake tunaona ikikosolewa na kuonekana kama inakosea inapotaka kutumia maarifa yake rejea dawa ya "Covid organics" ilivyopata upinzani kama kwamba Afrika haikuwa na dawa zake za aina yoyote na inapaswa kusubiri zinazoandaliwa na watu weupe.

Makanisani Afrika inafundishwa utamaduni mwingine kabisa leo hakuna ngoma,hakuna marimba, hakuna matari hakuna asili yoyote ya Africa Kanisani kwani tunaimba kizungu, tunasali kizungu tunaabudu kizungu jambo linalofanya uasili wetu kushindwa kupumua.

Pumzika George umetuwakilisha vizuri kwenye safari yako. Hatupumui vizuri ila tunapambania uhai bado chini ya goti la mkandamizaji.
Wakulaumiwa ni watawala wa kiafrica na sio mtu mweupe hapo.Adui wa mwafrika ni mwafrika mwenzake
 
Back
Top Bottom