"Nashindwa kupumua" ni sauti ya Afrika kwa ujumla, George Floyd ni sampuli

Waafrika bado tuna safari ndefu sana. Ukiacha kukandamizwa na mtu mweupe sisi wenyewe tunakandamizana. Mfano hapa Tz Ukandamizwaji unaofanywa na wenye mamlaka ni mkubwa zaidi kuliko unaofanywa na mzungu.
Nadhani wote mnajua kinachoelendelea dhidi ya upinzani.
Marekani rate ya mauaji ya black Vs Black ni ya hali ya juu kuliko hata White Vs Black.
South Africa kuna Xenophobia,
Ukija Congo kuna waasi, Ukienda Somalia kuna vita ya kidini.
Kwa kifupi mtu mweusi hana sehemu ya kupumua ndio maana pamoja na ukandamizaji wote unaofanywa na mtu mweupe bado Waafrika wako radhi kuhatarisha maisha yao kukimbilia Ulaya kusaka Maisha bora
 
Achana na uyo mcheza pono ndege wa mbali wa nn, Tundu Lissu na Ben saa nane ndo vile pambania vya nyumbani kwako kwanza ndo uwende kwa jirani yako bablai
 
We Afrika umebaguliwa nani mbona unafikra za kitumwa sana
Kwa hiyo yalowahi tokea ndani ya Afrika kusini ndani ya miaka minne iloipita yale yalikuwa ni maigizo au filamu, umesahau ule usemi wa kama kusoma haujui basi hata picha huielewi ?
 
Kama ni wabaya mbona hata kuvaa chupi walikufundisha
We jamaa utakua ni crossbrees ya beberu na simbilisi katika hoja fikirishi kama hii huwezi kuandika utopolo huu bwa mdogo samahani siwezi kukuita mkuu
 



Mbona marekani wameuwa mamilioni ya watu duniani, huko libya kila siku wanakufa mpaka Raisi na kiongozi wetu pendwa Muamar gadafi kauawa dhidi ya marekani lakini hakuna aliepaza sauti si viongozi wala wadau mliomo humu!!!!! au huyo hakua mwafrika mwenzetu ndio maana mkampotezea!!!! Ila ya floyd kuuawa ndio imekua big issue na ina umuhimu zaidi ya wengine?? Mnachekesha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…