Nashindwa kuwaelewa Vodacom

Vodacom wanakula vifurushi vya wateja kwa kasi ya kutisha.

Ukiwapigia simu kuuliza kulikoni wana majibu yao tayari
1. Wanakwambia hapa tukiangalia hatuoni tatizo
2. Ukizidi kuuliza wanakwambia labda kuna background apps zinarun kwenye simu yako

Mimi nimeshawahama, situmii data zao tena siku hizi.

Ujanja ni kuhakikisha una line za mitandao tofautitofauti. Mtandao mmoja ukizingua hasa kwenye data unahama fasta, unakwenda kwenye nafuu
 
watumiaji wa vodacom ni matajiri, masikini tupo halotel.
 
Vodacom kiukweli simu zetu hazitendewi haki kwa mfano..... Napigiwa nikiwa hewani wala simu haitumiki lakini wanaonipigia wanasema sipatikani,Ujumbe mfupi ukitumwa haufiki wa wakati kiukweli inakera sana.
 
izi MB hizi sio kwa kasi hiyoo 😅😅😅 eti superspidi kumbe wizii MB zinaenda kama stopwatch. voda wezi


ova
 
Nasikia wamepata MD/CEO mpya.

Mahesabu yao yalikuwa mabaya kiasi kwamba Mwenyekiti wa bodi yao aliondoka!! Hivyo baada ya hapo nilitegemea kuwa CEO wao nae aondoke!!! Ntashangaa sana kama wafanyakazi hawotapunguzwa hivi karibuni.
 
Kuna uwezekano mkubwa ukawa Matumizi yetu ni makubwa lakini tatizo letu Kubwa Watumiaji huwa tunapenda zaidi Kulalamikia Kampuni hizi.
 
Asanteni nyote kwa mrejesho. Majumuisho niliyofanya ni kwamba Vodacom ni wezi, maana binafsi nimeumia sana. Kuanzia sasa sitanunua airtime wala data kwa Vodacom. Line utabaki kwa wanaonipigia. Bye bye Vodacom!
Kuna uwezekano mkubwa ukawa Matumizi yetu ni makubwa lakini tatizo letu Kubwa Watumiaji huwa tunapenda zaidi Kulalamikia Kampuni hizi.
e
 
Kweli sasa hivi wanaiba mchana kweupe, kuna kipindi nilikuwa nanunua 3GB kwa wiki natumia hadi wiki inaisha, sasa hivi hizo 3GB, ni siku mbili tu, naambiwa kifurushi kimeisha, nilipo wapigia simu wakanijibu Sababu ni natumia 4G, ndo maana data zinaisha haraka
 
Mimi huwa naweka kifurushi cha Tshs 3,000/- Dk 245 Voda kwa Voda na dk 240 mitandao yote, kwa siku 7

*149*01# then 2 halafu 1

Sema nilichohizi kwenye hii mitandao, KILA MTU ANA MENU YAKE... unaweza usifanane kiwango na aina ya vifurushi na mwenzio.. Unaweza bonyeza namba zile zile lakini unachokipata wewe, ni tofauti na mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…