Nashindwa kuwaelewa Vodacom

Nashindwa kuwaelewa Vodacom

Vodacom wanakula vifurushi vya wateja kwa kasi ya kutisha.

Ukiwapigia simu kuuliza kulikoni wana majibu yao tayari
1. Wanakwambia hapa tukiangalia hatuoni tatizo
2. Ukizidi kuuliza wanakwambia labda kuna background apps zinarun kwenye simu yako

Mimi nimeshawahama, situmii data zao tena siku hizi.

Ujanja ni kuhakikisha una line za mitandao tofautitofauti. Mtandao mmoja ukizingua hasa kwenye data unahama fasta, unakwenda kwenye nafuu
 
watumiaji wa vodacom ni matajiri, masikini tupo halotel.
 
Vodacom kiukweli simu zetu hazitendewi haki kwa mfano..... Napigiwa nikiwa hewani wala simu haitumiki lakini wanaonipigia wanasema sipatikani,Ujumbe mfupi ukitumwa haufiki wa wakati kiukweli inakera sana.
 
izi MB hizi sio kwa kasi hiyoo 😅😅😅 eti superspidi kumbe wizii MB zinaenda kama stopwatch. voda wezi


ova
 
Nasikia wamepata MD/CEO mpya.

Mahesabu yao yalikuwa mabaya kiasi kwamba Mwenyekiti wa bodi yao aliondoka!! Hivyo baada ya hapo nilitegemea kuwa CEO wao nae aondoke!!! Ntashangaa sana kama wafanyakazi hawotapunguzwa hivi karibuni.
 
Nimekuwa nikitumia mtandao was Vodacom tangu mwaka 2000 na kwa ujumla nimekuwa nikiridhishwa na huduma. Lakini katika siku za karibuni nimeanza kutilia shaka huduma zake, hususan vifurushi vyao. Nasema kwa sababu siku hizi nikinunua kifurushi cha sh 2,500 kinachonipa dk 150 za kutumia wiki nzima, baada ya siku 2 au 3 na nikiwa nimepiga simu chache mara ujumbe kuwa kifurushi kimekwisha. Jambo hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara. Mwanzoni nilidhani ni nahati mbaya lakini naanza kupata shaka kwamba naibiwa, tena mchana kweupe. Swali kwa wale wanaotumia mtandao huu, je wapo ambao wanaoibiwa kama mimi?
Kuna uwezekano mkubwa ukawa Matumizi yetu ni makubwa lakini tatizo letu Kubwa Watumiaji huwa tunapenda zaidi Kulalamikia Kampuni hizi.
 
Asanteni nyote kwa mrejesho. Majumuisho niliyofanya ni kwamba Vodacom ni wezi, maana binafsi nimeumia sana. Kuanzia sasa sitanunua airtime wala data kwa Vodacom. Line utabaki kwa wanaonipigia. Bye bye Vodacom!
Kuna uwezekano mkubwa ukawa Matumizi yetu ni makubwa lakini tatizo letu Kubwa Watumiaji huwa tunapenda zaidi Kulalamikia Kampuni hizi.
e
 
Kweli sasa hivi wanaiba mchana kweupe, kuna kipindi nilikuwa nanunua 3GB kwa wiki natumia hadi wiki inaisha, sasa hivi hizo 3GB, ni siku mbili tu, naambiwa kifurushi kimeisha, nilipo wapigia simu wakanijibu Sababu ni natumia 4G, ndo maana data zinaisha haraka
 
Ujinga wa hivi vifurushi vya voda na kutoa dakika chache sana za kwenda mitandao mingine tofauti na hapo awali/mitandao mingine.

Kwa mfano,kifurushi cha wiki cha sh 2000(ofa maalumu) wanakupa dakika 150 za voda kwenda voda na dakika 15 tu za mitandao mingine. Hivyo, usipokuwa makini, unaweza kujikuta unazimaliza hizo dakika 15 ndani ya Siku moja au mbili wakati umenunua kifurushi cha wiki cha shilingi 2000 na ukilalamika watakwambia vigezo na mashariti vimezingatiwa.

Kifurushi hiki kina nafuu kwenye kutoa MB tu ambapo wanakupa GB moja utumie ndani ya hizo siku 7.
Mimi huwa naweka kifurushi cha Tshs 3,000/- Dk 245 Voda kwa Voda na dk 240 mitandao yote, kwa siku 7

*149*01# then 2 halafu 1

Sema nilichohizi kwenye hii mitandao, KILA MTU ANA MENU YAKE... unaweza usifanane kiwango na aina ya vifurushi na mwenzio.. Unaweza bonyeza namba zile zile lakini unachokipata wewe, ni tofauti na mwingi
 
Back
Top Bottom