OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Leo asubuhi niliacha simu imezagaa zagaa bila kuifunga. Niliporudi nikakuta Afisa Upelelezi anaifanyia upekuzi wa kina bila kibali. Ikabidi nimtazame machoni kiwiziwizi kuona kama kuna chozi linalenga lenga. Sikuona chozi ila nikaona ni kama mtu anayevuta kumbukumbu fulani. Ikabidi nitoke nje kupanga mbinu ikiwa nitadakwa na kashfa yeyote basi nije na uongo gani. Lakini pia kukumbuka kama kuna sms nilisahau kufuta maana huu uchunguzi umekuja ghafla.
Baada ya muda nikaona ameendelea na mambo mengine. Nikajua hapa kuna amani, nikarudi. Akaniambia "Bahati yako leo, ila nitakukamata tu! Simu yako ile pale"
Daah nashukuru nimeanza mwaka kwa bashasha bila makandokando. Kwa hiyo nimeanza mwaka na kafeeling fulani kapekuliwa simu halafu usikutwe na umalaya wowote.
Aidha safari hii shetani amezembea kuniharibia amani.
Heri ya Mwaka Mpya Wakuu