Nasikia harufu ya Chid Benz kurudi tena kwenye chat

Walaiiiiii..... 🤣 🤣
 
Chid ni yule yule, mkali siku zote, shida unga, aache unga mtamuona chid yule yule wa mashaallah, daresalaam stand up n.k.

Alikuja na muda ft q chief, mbona ngoma ilikuwa kali tu, shida unga, aache madawa, ndioa adui wake.
Muda feat Chila haikufanya poa kwa sababu Chidy alivaa uhusika wa victim. Tangu lini wabongo wakapokea ngoma ya victim? Hata yeye mwenyewe alisema alifanya makosa makubwa sana kufanya ngoma kama ile kwa sababu ilimfanya atie huruma zaidi na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wa kibongo huwaga hawampokei artist anae kuja na ngonjera za kutia huruma
 
Kufanya poa, mie naona ilifanya poa, sijui upoa gani, na mashabiki wa muziki waliipokea vizuri tu. Inawezekana ikawa kweli haikupokelewa vizuri sina ushahidi wa hili.

Mie sikuzungumzia kufanya poa, mie nimezungumzia ngoma ilikuwa kali.
Ngoma ilikuwa kali, chidi alifanya vizuri saana

Pia q chief alikuja na ngoma ile ya namtafufa, ikawa kali na ikapokelewa japo alitia huruma na matukio yake,
 
Wabongo nyimbo za kutia huruma hawazitakagi kabisa. Ukiimba nyimbo za kutia huruma kwa wabongo unakuwa unajichoresha tu. Wabongo wanapenda mtu anae vimba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…