Mkuu hawa panya usiseme hivo, ni zaidi ya tatizo! Kuna mdogoangu nae ni kijana wa hovyo, anaishi kwa mama sio mbali na nyumbani kwangu siku moja amekuja kwangu usiku akanigongea vzr tu akaingia tukawa tunaongea lakini akaniambia yuko na wenzake wachake wapo nyuma ya nyumba wamekaa kwamba nisiwe na wasi, akatoka kwenda kukaa nao'
Nikawa nasikia sauti chache za chinichini, nikakadiria labda kuna watu hawazidi 6, nilivotoka nusu nizimie! Nilikuta kuna watu kama 30 na zaidi! Na huwezi amini hakuna hata moja ninaemjua zaidi ya huyo dogo tu!
Na kila muda anatoka mmoja akirudi anakuja na wengine tena! Mpaka wanaondoka pale mida ya saa sita usiku wameshakuwa wengi mnooo!
Dogo akawa ananitambulisha' nikagundua wantokea kiwalani, mbagala, wengine bunju nk.
Kesho yake nikasikia tukio la ajabu!
Wale madogo ukiwa unaongeanao ni wana heshima saana! Na wako wazi hawafichi kitu.
Ila wakati wanaondoka niliwaambia pale wasije tena. Wakasema "heshima kwako bro popote tukikuona tutakulinda"
Kuwazibiti panya inatakiwa weledi tofauti kbs na hizi operation za polisi.