Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Kwa taarifa yako sasa,juzi aliuwawa mmoja wa hao panya road,jana mchana wakati anazikwa wakaja field force gari si chini ya4,vijana wakakimbia,wakakamatwa baadhi,na maiti police wakasaidia kuzika..
Jana hiyo hiyo Usiku hao vijana wakajiorganize tena wakawa wanapita mitaani kulipiza mwenzao kuuwawa ..
Ila kuna baadhi wametiwa mbaroni...
Over and out mkuu....
Imefikia hatua hata ugomvi wa vijana mtaani wakigombea demu ukitokea mnasema Panya Road acheni kutia watu hofuYombo Kipera kuna mtaa unaitwa Kinyantira
Mkuu huo ndio kweli,yani hata ukimpiga mkeo tu utasikia panya road wamempiga MdadaImefikia hatua hata ugomvi wa vijana mtaani wakigombea demu ukitokea mnasema Panya Road acheni kutia watu hofu
Yombo hayo ndio maisha yao vijana wa uko,nakumbuka kama miaka mitatu iliyo pita tulizika na madifenda pale makabuli ya site (Dovya).Yombo Kipera kuna mtaa unaitwa Kinyantira
tumechoka na kelele zenu, nawashauri kila mwanaume mtaani anunue moja ya hizi nyenzo pamoja na firimbi.
Wakija hao watoto piga firimbi kila mtu atoke na shoka au panga lake. Ni kukata na kufunua tu hakuna kuchukua mateka.
View attachment 2221710
View attachment 2221711
Kuwa makini huyo dg usikubar akuletee wauni itakucost trust me utakuja jikuta nyuma ya nondoMkuu hawa panya usiseme hivo, ni zaidi ya tatizo! Kuna mdogoangu nae ni kijana wa hovyo, anaishi kwa mama sio mbali na nyumbani kwangu siku moja amekuja kwangu usiku akanigongea vzr tu akaingia tukawa tunaongea lakini akaniambia yuko na wenzake wachake wapo nyuma ya nyumba wamekaa kwamba nisiwe na wasi, akatoka kwenda kukaa nao'
Nikawa nasikia sauti chache za chinichini, nikakadiria labda kuna watu hawazidi 6, nilivotoka nusu nizimie! Nilikuta kuna watu kama 30 na zaidi! Na huwezi amini hakuna hata moja ninaemjua zaidi ya huyo dogo tu!
Na kila muda anatoka mmoja akirudi anakuja na wengine tena! Mpaka wanaondoka pale mida ya saa sita usiku wameshakuwa wengi mnooo!
Dogo akawa ananitambulisha' nikagundua wantokea kiwalani, mbagala, wengine bunju nk.
Kesho yake nikasikia tukio la ajabu!
Wale madogo ukiwa unaongeanao ni wana heshima saana! Na wako wazi hawafichi kitu.
Ila wakati wanaondoka niliwaambia pale wasije tena. Wakasema "heshima kwako bro popote tukikuona tutakulinda"
Kuwazibiti panya inatakiwa weledi tofauti kbs na hizi operation za polisi.