Nasitisha kwa muda kushabikia Simba Sports Club ila wakiyafanyia kazi yafuatayo nitarudi!

Nasitisha kwa muda kushabikia Simba Sports Club ila wakiyafanyia kazi yafuatayo nitarudi!

Simba imeangushwa sana viongozi hasa huu uongozi wa kina Aveva (jamaa kawekwa kama boksi) hana maamuzi yeyote
Hans Pope anapaswa kuondolewa kwenye hiyo kamati ya usajili ndio anaongoza kuiharibu klabu ya Simba
 
halafu uongozi wasiwe bahiri watambue kuwa sasa hivi pesa pia inahusika kwe soka,angalia yale kina kamusoko ya yanga sijui wengine wanaitwa ngoma tunaonaga yanapga kazi kinoma,sasa c simba na timu letu la shiling mia lile inakuwa kazi kidogo..yaan simba kila cku utata ni usajili tu hasa wachezaji wa nje wengi huwa tunachemka kwan wakija huwa hawafany vizur,okwi pale tuliwin ila wengine amna kitu.........nawapongeza azam na yanga hata kama wamebutuliwa huko kimataifa ila usajili wanaofanya inaonyesha kweli jamaa wako serious kujenga timu yao..simba tunaishia kuish kwa historia tu ohh tunafunga waarabu mara cjui nn badala ya kusajili wachezaji wenye hazdhi ya kuchezea simba,simba sasa kama arsenal upumbafu mtupu

Kuna wachezaji fulani niliona Simba inawavizia ili iwasajili msimu ujao washambuliaji wawili mmoja kutoka Toto na mwingine wa Cost Union na mchezaji mwingine sijui wa wapi alitolewa kama mkopo.Nilihuzunika kweli,kwa sasa Simba inahitaji washambuliaji kama wawili na viuongo wazuri kama watatu kutoka nje ya nchi.

Kavumbagu naye nasikia Simba wanataka kumchukua.Kama ni kweli basi huyo Aveva na wasaidizi wake waondolewe mapema sana kabla hawajaharibu katika usajili wa msimu ujao.Aveva ni alama ya kushindwa na hajui afanyalo...
 
kwa kweli uongozi huu wa simba ulioingia kwa mbwembwe umetupa maumivu makali si mashabiki wa simba damu. mara tu baada ya kupoteza dira kwenye kutafuta ubingwa ghafla wameanza hadithi zao kwenye magazeti kama kawaida mara okwi anakuja, mara mavugo kashasajiliwa, mara tunataka kumrudisha miraji adam na yule fowadi wa wa toto african aliyewafunga goli. mi nafikiri kwa heshima na taadhima viongozi wawe waungwana wajiuzulu waitishe uchaguzi ili waingie viongozi wenye uwezo. soka sasa hivi ni sayansi. simba ingekuwa timu tishio iwapo ingeacha usanii. ilikuwa na hazina ya vijana wangewapa mikataba mirefu mizuri yenye maslahi, mishahara mizuri posho nzuri na mortisha halafu wangeongeza wageni na wazoefu wachache. hisia zangu ni kuwa kwenye usajili wa wachezaji wa kigeni kuna watu wanafaidika kwenye pesa ya usajili na mshahara ya hao wachezaji. kwa mfano kwa sasa mchezaji wa kigeni anyestahili kucheza simba ni murshid kidogo na majabvi hao wengine nikipita kwenye ndo ndo cup napata wanalingana viwango na wao. pia viongozi wajichunguze wenyewe kwa wenyewe kama kweli ni wamoja na hamna hujuma kati yao.
 
Mimi nimepotezea morali na timu yangu simba sport club,viongozi matapeli tu
 
...nashangaa sana,kuna kiongozi mmoja wa Simba kila siku utamsikia Yanga wanapendelewa,mmeshindwa kabisa kutengeneza timu mmeamua kugeuka kulia lia tu sababu mnajua wengi wa mashabiki hamna kitu kichwani,wataamini kila ujinga mnaoongea!,

Halafu jingine,hivi ni kwanini haswa hawa jamaa waligoma kumpa Dewji timu?!, wanadai pesa alizotaka kuzitoa Dewji ni ndogo,wakati wao hata pesa za usajili wa maana hawana,kila siku kuokota wachezaji toto,jkt ruvu, na nyingine,km timu imewashinda si muwaachie wengine,kumbe issue Simba ni kichaka cha kupiga pesa!

Simba haitakaa ichukue ubingwa chini ya huu uongozi wa matapeli uliopo,majitu yanayoinyonya klabu,badala ya kuipeleka timu mbele,na hii yote pia inachangiwa na wanachama wanapopiga kura kuchagua viongozi,huwa wanaongozwa na mihemko sana,wacha tuisome namba!
 
Simba imeangushwa sana viongozi hasa huu uongozi wa kina Aveva (jamaa kawekwa kama boksi) hana maamuzi yeyote
Hans Pope anapaswa kuondolewa kwenye hiyo kamati ya usajili ndio anaongoza kuiharibu klabu ya Simba
Mbaya anakuwa Yanga eti ananunua mechi khaaa...............
 
Mbaya anakuwa Yanga eti ananunua mechi khaaa...............

Angalia hiyo kamati ya Hans Pope ilivyochemshaa kwenye usajili wa wachezaji na kufukuza makocha.Unamuacha Tambwe wakamsajili Serunkuma akachemsha eti wakamrudisha Mgosi ,striker ambaye hajafunga hata goli
 
kwenye usajili viongozi wa simba bado sana na mara nyingi wanakuwa kama arsene wenger. wanawajua wachezaji wazuri na wanafanya na mazungumzo ya awali lakini mwisho wa siku wanasajiliwa na timu nyingine. bila usajili makini na wa kisayansi na kuinua vijana wachache waliolelewa timu B simba isahau mafanikio. hivi inashindikana nini kuunda kamati ndogo tu ya wachezaji wazamani kama 10 waliochezea simba kwa moyo wawafanyie kazi ya scouting kama kamati ya usajili imeshindwa kazi?
 
Kwan zile hela za usajili wa okwi na ile percent ya samata uongozi umepeleka wapi maana zinatosha kutengenezea miundombinu,pitch, hostel nzuri. pale mbunju.
 
Nafikiri uongozi wa aveva unatakiwa ukaepembeni hakuna chochote walichofanya hata Kombe la fa simba wameshindwa kuchukua wampishe mzee dalali au rage
 
kwa mfano kwa sasa mchezaji wa kigeni anyestahili kucheza simba ni murshid kidogo na majabvi hao wengine nikipita kwenye ndo ndo cup napata wanalingana viwango na wao. pia viongozi wajichunguze wenyewe kwa wenyewe kama kweli ni wamoja na hamna hujuma kati yao.
Sawa kabisa.Foward wakimpata Okwi,Mavugo na yule mshambuliaji wa Tusker kama sijakosea au hata type yao it's ok.Katikati iwapate wachezaji watatu type ya akina Echesa zamani hizo.Wengine tutapata humuhumu,ila inabidi kuangalia sana.mf mabeki inabidi wawe kama washambuliaji kama Kapombe au Juma Abdul.Vinginevyo tutakuwa wasindikizaji miaka nenda rudi hadi Aveva aondoke.
 
Hapo kwa ka Alcohol na Juma abdul mbona mna kijana kariba yao tena bado mdogo kabisa anaitwa hasan kessy mmempeleka wapi kwani?
 
Sawa kabisa.Foward wakimpata Okwi,Mavugo na yule mshambuliaji wa Tusker kama sijakosea au hata type yao it's ok.Katikati iwapate wachezaji watatu type ya akina Echesa zamani hizo.Wengine tutapata humuhumu,ila inabidi kuangalia sana.mf mabeki inabidi wawe kama washambuliaji kama Kapombe au Juma Abdul.Vinginevyo tutakuwa wasindikizaji miaka nenda rudi hadi Aveva aondoke.

Okwi yupi huyo,yule yule wa siku zote tunaemfahamu au Okwi mpya kutoka Nigeria?kweli Simba mmelogwa,ndio yale yale ya kumsajili Mgosi.
 
Juzi Mo Deuj anaomba auziwe sgd United baada ya kutinga daraja la kwanza.Hata kama hatumwamini,ila simba ni timu kubwa yenye uwezo wa kumpa faida kimatokeo.
 
Back
Top Bottom