Nasitisha kwa muda kushabikia Simba Sports Club ila wakiyafanyia kazi yafuatayo nitarudi!

Nasitisha kwa muda kushabikia Simba Sports Club ila wakiyafanyia kazi yafuatayo nitarudi!

Kumbe Jery Muro anawaumiza wengi!
Point namba 12 inaonesha kama umetumwa na Dewj, na point 15 inaonekana nawewe pia unapenda majungu...anyway kama umechoka kukaa matopeni karibu kwa wa kimatafa.
 
Kumbe Jery Muro anawaumiza wengi!
Point namba 12 inaonesha kama umetumwa na Dewj, na point 15 inaonekana nawewe pia unapenda majungu...anyway kama umechoka kukaa matopeni karibu kwa wa kimatafa.
Tulia wewe. Wa kimataifa mna rekodi gani? usilete akili za jerry muro
 
Tulia wewe. Wa kimataifa mna rekodi gani? usilete akili za jerry muro
Kwa bahati nzuri sikuwa nazungumza nawewe, punguza tabia za kike kudaka maneno yasiyokuhusu..oooh sorry nilisahau kama hii ni tabia yenu wamatopeni..hata wewe kama umechoka kuishi matopeni tunakukaribisha huku lkn plz ukija tabia za huko ziache hukohuko huku ni soka tu tena la kimataifa siyo mabonanza
 
Kwanza nikiri kabisa kuwa nimekuwa ni Mshabiki, Mpenzi na nashukuru Mwenyezi Mungu kila mara moyo wangu umekuwa mgumu sana Mimi kuchukua kadi ya Uanachama ya Klabu ya Simba kwani hapa tu siyo MWANACHAMA naumia hata nataka KUFA kwa Presha je ingekuwaje kama ningekuwa MWANACHAMA halali wa Simba?

Japo sijawa bado Mwanachama ila nikiri kuwa NIMEKUWA nikishiriki katika shughuli mbalimbali za kuifanikishia Simba ushindi huko nyuma na hata kwa miaka hii minne ( 4 ) huu sasa unaenda wa tano ( 5 ) nimeteseka sana juu ya Simba kwa kuingia takribani michezo yao mingi, kuchangia pale nilipoweza na kutoa ushauri wa kuisaidia timu lakini NASIKITIKA kusema kuwa juhudi zangu hazijasaidia kwa sababu ambazo nitaziweka baadae humu.

Nakumbuka jinsi nilivyochuma dhambi za UWONGO kwa kudanganya OFISINI kwangu hasa kwa Mabosi zangu kuwa NAUMWA au nina UDHURU ilimradi tu nipate ruhusa niende kutizama mechi za Simba Taifa na hadi Mikoani.

Nina MASIKITIKO makubwa na HASIRA kali sana kwa jinsi timu yangu ya Simba inavyoendeshwa sasa na LEO NAOMBA NITOE MAAMUZI YANGU HAYA MAGUMU KUWA NASITISHA RASMI KUISHABIKIA NA KUJIHUSISHA KWA LOLOTE LILE LINALOIHUSU TIMU YA SIMBA SPORTS CLUB KUTOKANA NA UPUUZI KAMA SIYO UNAFIKI HUU NINAOUWEKA HAPA:

  1. Timu ya Simba kwa sasa INAONGOZWA KIHUNI TUPU.
  2. Timu ya Simba kwa sasa VIONGOZI WAKE WAKUU Rais na Makamu HAWAPATANI.
  3. Timu ya Simba kwa sasa IMEKUWA KAMA MBUZI WALIOKOSA MCHUNGAJI.
  4. Timu ya Simba kwa sasa IMEWEKEZA KATIKA UCHAWI NA MAJUNGU BADALA YA SOKA.
  5. Timu ya Simba kwa sasa INA WANACHAMA WANAFIKI NA NDUMILAKUWILI.
  6. Timu ya Simba kwa sasa HAIWAJALI TENA WACHEZAJI WAKE HASA KIMASLAHI.
  7. Timu ya Simba kwa sasa NDIYO INAZIDI TU KUPOTEZA DIRA KIMAENDELEO.
  8. Timu ya Simba kwa sasa IMEWEKEZA KATIKA UJINGA NA UPUMBAVU TUPU.
  9. Timu ya Simba kwa sasa INA LAWAMA NYINGI BADALA YA KUWAJIBIKIA YENYEWE.
  10. Timu ya Simba kwa sasa INA WIVU WA KITOTO NA USIO NA TIJA KISOKA.
  11. Timu ya Simba kwa sasa INATAWALIWA NA WANACHAMA WAHUNI NA WASANII TUPU.
Endapo yatafanyika haya yafuatayo NITASHAWISHIKA tena kurudi kuishabikia timu ila kwa sasa nahitaji kupumzika kwani NIMETESEKA na KUHANGAIKA mno na Simba Sports Club bila MAFANIKIO :
  1. Kufanyike MKUTANO wa DHARURA na timu akabidhiwe Mo Dewji aisuke upya timu.
  2. Wachezaji wote wa Simba wapewe STAHIKI zao bila vitisho au kudhulumiwa.
  3. Utaratibu wa timu kuwa chini ya MATAWI yanayoongozwa na Watu WAHUNI, WAONGO na wenye NJAA ukome.
  4. Makamu wa Rais Kaburu na Mjumbe wa Simba Tully WATUBU kwa Wanasimba kwa kuwa VIBARAKA wa Yanga na kuwa na MAHABA na timu ya Yanga. ( Ushahidi wa haya kuwa Kaburu na Tully ni Yanga damu 100% upo na siku si nyingi nitaweka kila kitu HADHARANI )
  5. Timu iache kuwekeza sana katika KUFANYA au kupenda USHIRIKINA kuliko kuijenga timu Kisayansi zaidi ili ipate matokeo mazuri.
  6. Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara AACHANE NA TABIA YA KILA MARA KUISEMA au KUISHAMBALIA Yanga kwa GHARAMA za UOZO wa Simba wenyewe na badala yake AJIKITE KATIKA KUSEMA UKWELI WA YALE TU YAHUSUYO Simba bila kuwa na UWOGA wowote.
  7. Rasilimali za Simba ziwanufaishe kwanza Wachezaji na pili MAENDELEO ya Klabu ya Simba.
  8. Kamati zote zilizoteuliwa ndani ya Klabu ZIVUNJWE RASMI na Kamati ya UTENDAJI tu ya Simba ndiyo IWAJIBIKE katika kuiongoza timu ya Simba.
  9. Kufanyike UCHUNGUZI wa KINA sana kuweza kujua ni akina nani wapo ndani ya Klabu ya Simba Sports Club lakini WANATOA SIRI ZOTE za Simba kwa WAPINZANI wetu Yanga na bahati nzuri WANAJULIKANA sana.
  10. Wanachama na Mashabiki wa Simba TUACHE KUWA MAZUZU NA MAJUHA wa KUDANGANYWA kila mara kwa maneno matamu au kauli tamu tamu na TUNARIDHIKA huku timu INAANGAMIA.
  11. Timu ya Vijana ya Simba B ipewe UMUHIMU MKUBWA SANA na KILA AINA YA MSAADA INAYOITAKA na ikiwezekana iwe chini ya Makocha ambao walikuwa Wachezaji wetu mahiri wa Simba ili waweze kutujengea Kikosi thabiti cha Vijana ambacho kitakuja kutusaidia baadae na hata kutupunguzia gharama zisizo za lazima za kusajili WACHEZAJI MAJIPU wa KIGENI ambao hawana tofauti na Wafanyakazi hewa kutokana na kwamba gharama zao za USAJILI haziendani na aina yao ya Soka kama Wachezaji wa kigeni.
Naomba RADHI / MSAMAHA sana kwa Wana Simba Sports Club wenzangu ambao kwa namna moja au nyingine BANDIKO hili au UZI wangu huu UTAWAKWAZA ila kama kawaida au asili yangu huwa SILEI UPUUZI, UJINGA na UPUMBAVU pale ninapouona ila kwa Viongozi wa Simba Sports Club watakaousoma basi naomba WAJIFUNZE kitu na wajitahidi kufanyia kazi mapungufu niliyoyaainisha hapo juu.

NB: Tumechoka sasa kila kukicha kubatizwa kusikokuwa rasmi kwa kuitwa :

  • Wa Mchangani
  • Wa Matopeni
  • Wa Hapa hapa
  • Wa Kunawa lakini asiyekula chakula
  • Bingwa wa Kuoa lakini mbovu wa kuzalisha
  • Kubwa jinga halafu hovyo
  • Baiskeli ya miti
  • Simba wa mjini
  • Wakurupukaji
  • Wa Mabonanza
  • Masikini wa akili
Nawatakieni kila la kheri wale wote ambao bado mnaendelea kuwa na imani kuwa Simba Sports Club ITAKUWA BINGWA msimu huu wa 2015 / 2016 na wale ambao bado mnajipanga kuhudhuria mechi za Simba nne ( 4 ) zilizobaki ILA kwa Mimi binafsi NASIMAMA RASMI KUJIHUSISHA KWA LOLOTE au CHOCHOTE juu ya Simba Sports Club.

Akhsanteni na naomba kuwasilisha.

Mkuu umesahau kitu kimoja! Tatizo la simba ni mwenyekiti Aveva, Mimi nilipumzika kushabikia simba Mara baada ya huyu mwenyekiti kuwafukuza uanachama waliokuwa wapinzani wake kwenye uchaguzi, badala ya kujenga yeye akabomoa, ndicho kinachoitafuna simba hadi Leo, "dhambi ya ubaguzi"
Hakuna lolote linaloweza kufanikiwa simba kwa sasa mpaka mwenyekiti huyu atoke!
Tangu aingie hakuna kombe wala kushiriki michuano ya klab bingwa
 
Hapo kwa ka Alcohol na Juma abdul mbona mna kijana kariba yao tena bado mdogo kabisa anaitwa hasan kessy mmempeleka wapi kwani?
Kawaida yao kutupa almasi wakijua ni vipande vya chupa.
Kessy huyo mbioni kutua Yanga akifuata nyayo za Yondani na Tambwe.
Simba sasa ni nursery ya kuzalisha wachezaji ili waende Yanga au Azam
 
Kwa bahati nzuri sikuwa nazungumza nawewe, punguza tabia za kike kudaka maneno yasiyokuhusu..oooh sorry nilisahau kama hii ni tabia yenu wamatopeni..hata wewe kama umechoka kuishi matopeni tunakukaribisha huku lkn plz ukija tabia za huko ziache hukohuko huku ni soka tu tena la kimataifa siyo mabonanza
Jibu hoja acha kurukaruka kama umekalia dole gumba
 
pole mkuu sisi wengine tulishatoka zamani na roho zimetulia tatizo la simba ni azam toka iwe strong hatujawahi fulukuta tunaishia nafasi ya 3 kumbuka mpaka sasa simba tumekuwa tunapoteza point kwa azam,yanga +toto na hakuna kiongozi mwenye mkakati kututoa hapo
 
Kawaida yao kutupa almasi wakijua ni vipande vya chupa.
Kessy huyo mbioni kutua Yanga akifuata nyayo za Yondani na Tambwe.
Simba sasa ni nursery ya kuzalisha wachezaji ili waende Yanga au Azam

Kessy haiwezi kuchukua no.ya Juma Abdul.
 
Okwi yupi huyo,yule yule wa siku zote tunaemfahamu au Okwi mpya kutoka Nigeria?kweli Simba mmelogwa,ndio yale yale ya kumsajili Mgosi.

Utakuwa unamuogopa tu Okwi,unaijua habari yake vizuriOkwiiiiiiiiiiiii!!!
 
Kessy haiwezi kuchukua no.ya Juma Abdul.
Hilo ni kweli lakini endapo Abdul ataumia, Kessy atakuwa ni sub nzuri sana. Pia anaweza kutumika kwa njia nyingine kama winger. Lengo ni kuwa na kikosi kipana. Kuna kuumia, matizo ya kifamilia na kutumikia kadi za njano au nyekundu.
 
Hilo ni kweli lakini endapo Abdul ataumia, Kessy atakuwa ni sub nzuri sana. Pia anaweza kutumika kwa njia nyingine kama winger. Lengo ni kuwa na kikosi kipana. Kuna kuumia, matizo ya kifamilia na kutumikia kadi za njano au nyekundu.

Kama anaenda kusubiri mtu aumie hapo sawa ila si kikosi cha kwanza.Kwanza hana cross nzuri maana cross zake nyingi anapiga kwa gollkeeper japo ni mzuri kusukuma mashambulizi mbele,tatizo mtu wa kati anaposubiri cross yake ndo utashangaa.
 
Simba imeangushwa sana viongozi hasa huu uongozi wa kina Aveva (jamaa kawekwa kama boksi) hana maamuzi yeyote
Hans Pope anapaswa kuondolewa kwenye hiyo kamati ya usajili ndio anaongoza kuiharibu klabu ya Simba
Ha ha ha wamatopeni bwana? Mwiteni Michael Wambura!
 
kwa shabiki wa kweli wa simba akisikia Kessy kaenda yanga sidhani kama atasikitika kwa mambo aliyotufanyia kwenye zile mechi mbili tulizopoteza pointi 6 muhimu.
 
kwa shabiki wa kweli wa simba akisikia Kessy kaenda yanga sidhani kama atasikitika kwa mambo aliyotufanyia kwenye zile mechi mbili tulizopoteza pointi 6 muhimu.

Halafu yule mtoto ni mbishi wa asili sijui wa wapi yulee sijui kala maharage ya wapi yulee,waondoke na Banda wake.Pale Simba kunastahili kubaki wachezaji kama 8 tu wengine ni wa kupiga chini.
 
Back
Top Bottom