Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila mkuu labda kwa upande mwingine, nadhani tunatofautiana pale ambapo unajaribu kuonesha kuwa Nasra ambaye tayari alishakuwa victim, may be ndiye alitakiwa kujitafutia msaada wa kisaikolojia. Kumbuka, wakati huo tayari alishakuwa psychologically compromised. Kama ni kweli, basi mume na ndugu ambao walimwona mtu anabadilika sana kutoka kwenye hali yake ya kawaida na hawakuchukua hatua wanabeba shea kubwa ya lawama!!
Babu DC!!
Mie siku zote huwa naamini mwanamke aliyeko kwenye ndoa anajiheshimu, anamuheshimu mumewe, anawaheshimu ndugu wa mume na wake pia, ukikuta mwanamke kabadilika mara nyingi chanzo ni mume wake, wanaume wanachangia kwa asilimia nyingi kubadilisha tabia za wake zao,
matatizo yanapotokea ndani ya ndoa sio wote wanaweza kuyamaliza kwa njia za busara babu DC, angalia mf. wa Nasra, kamfumania mumewe na njia pekee aliyoona itamwondolea machungu yake ni kulipa kisasi kwa kuwa na mwanaume mwingine, simlaumu manake hapo ndipo akili na maarifa yake yalipoishia. Mwingine labda angeamua kulewa wakati hapo kabla hakuwahi kutumia kilevi chochote, mwingine labda wangekaa wayazungumze then wasameheane na maisha yasonge... Hapa pia inabidi kumpata mume wa Nasra na kumuuliza ni kwanini aliamua kutoka nje ya ndoa yake... Usishangae pia akikwambia chanzo ni mke wake..
Babu DC ndoa zina siri nyingi usione milango na madirisha ukafikiri kuna amani sana!
Nasra alimkosea heshima mumewe, ila pia hakustahili kufanyiwa ukatili wa namna ile...ndoa ni ngumu babu DC, mie hata nashindwa nimtete yupi...
Kitu mura mbuya saguru ghati! haya kina mwita chacha,wankuru,ni mambo gani haya mnafanya?
Soma tena hiyo quote yangu paragrafu ya pili mstari wa mwisho....HIVI ULISHAJARIBU PIA KUJIULIZA SABABU ILOMFANYA HUYO MWANAUME ATOKE NJE YA NDOA, USIKIMBILIE KUTETEA JINSIA TU.. WANAWAKE wengine ndani ya nyumba wanamadhila hadi hupelekea mme kutafuta relief elsewhere unajuaje kama huyo nasra alikuwa ampalii huyo jamaa wakati wako ndoani!!?? Ishaonekana mwanaume ni mkimya sio varuvaru kama huyo nasra huoni hilo lilimfanya areact kimyakimya kwa kutafuta ahueni nje huko???
USILAZIMISHE CHANZO NI KUFUMANIWA KWA JAMAA.. JE WAJUA NINI KILIMPELEKEA AKAENDA NJE????
Hapa tunaenda pamoja jG, ni kweli Nasra hakutumia njia bora kumaliza tatizo lake!...Sijasema hivyo sl...
Naamini kulikuwa na njia bora zaidi kuliko kulipa kisasi...
Ila pia naamini unakubali kuwa "Mwanamke mwerevu huijenga nyumba yake na mpumbavu huivunja"
Ni kweli ila kutokufikiria huko kulisababishwa na nini? Mume aathiriwe na nini wakati yeye ndie kafumaniwa?... Hapa wote wawili walikosa busara, ila ukumbuke mioyo yetu ni tofauti yaezekana Nasra alishindwa kulipokea tatizo na kujipa muda wa kufikiri,..amini nakwambia alichokuwa anakifanya Nasra ni kujipooza maumivu alokuwa nayo...
Maamuzi ya Kuua hayapaswi kufanywa na binaadamu yeyote yule hata mwenzio awe amekukosea vipi. Huyo bwana alikosea tu hamna kitu kitakachomsafisha kwa kitendo alichofanya.
Hebu basi tupe misingi ya kisheria basi...Kwa nini unadhani kesi inaweza kutupwa na DPP (Nolle presequi)?
Mbona aliodoka sehemu ya tukio, halafu akarudi tena? Hii haiwezi kujenga mazingira kwamba alienda pembeni akakaa na kupanga kitu cha kufanya?
Hapa itabidi niwatafute maloya (lawyers) wanipe mwanga kidogo!!
Babu DC
Mie siku zote huwa naamini mwanamke aliyeko kwenye ndoa anajiheshimu, anamuheshimu mumewe, anawaheshimu ndugu wa mume na wake pia, ukikuta mwanamke kabadilika mara nyingi chanzo ni mume wake, wanaume wanachangia kwa asilimia nyingi kubadilisha tabia za wake zao,
matatizo yanapotokea ndani ya ndoa sio wote wanaweza kuyamaliza kwa njia za busara babu DC, angalia mf. wa Nasra, kamfumania mumewe na njia pekee aliyoona itamwondolea machungu yake ni kulipa kisasi kwa kuwa na mwanaume mwingine, simlaumu manake hapo ndipo akili na maarifa yake yalipoishia. Mwingine labda angeamua kulewa wakati hapo kabla hakuwahi kutumia kilevi chochote, mwingine labda wangekaa wayazungumze then wasameheane na maisha yasonge... Hapa pia inabidi kumpata mume wa Nasra na kumuuliza ni kwanini aliamua kutoka nje ya ndoa yake... Usishangae pia akikwambia chanzo ni mke wake..
Babu DC ndoa zina siri nyingi usione milango na madirisha ukafikiri kuna amani sana!
Nasra alimkosea heshima mumewe, ila pia hakustahili kufanyiwa ukatili wa namna ile...ndoa ni ngumu babu DC, mie hata nashindwa nimtete yupi...
Anhaa hiyo ndio point yako...!!
Labda kama tunaupungufu wa taarifa katika hii hadithi, ila kwa jinsi ulivyoeleza ni kuwa Mwanaume alirudi na kuwa mpole ndio "dada yetu" akapamba moto.....
Silengi kutetea upande wowote, au kuhalalisha kwa upande wowote ndio maana kama utakumbuka ulipoleta hii stori mwanzoni tu nilimlaani huyo "Kaka" kuwa "nyumba ndogo imefanya mambo"....
Leo baada ya kupata upande wa pili wa hadithi nimejaribu kutoa mawazo ya jumla kuwa katika nyumba kwa mujibu wa maandishi ya kidini yangu (japo kwa ufinyu) Mwanamke ana nafasi ya pekee sana katika kusimamia nyumba yake na familia....
Pamoja na u-victim wa dada Nasra ila tatizo rasmi limeanzia pale alipojaribu kulipiza kisasi, na yeye akatengeneza Victim mwingine "mumewe"... Sasa tukitaka kujenga hoja za nani ni Victim na alistahili nini basi wote ni victim!
Ndio maana nikaona kuwa turudi kwenye msahafu sahihi wa maisha (inaweza kuwa dini au asili yetu waafrika).....
- Nini majukumu ya wanawake kwenye familia na nafasi zao?
- Nini majukumu ya wanaume kwenye familia na nafasi zao?
NB: Tatizo limeshatokea, kujenga hoja kwamba nani ana makosa au nani alionewa inaweza isiwe na utamu sana Babu, tusaidiane kuelimishana namna bora katika ujenzi wa familia kama enzi zenu za miaka ya 47....
Bado naamini katika nafasi ya pekee ya Mama zetu katika kujenga Familia yenye furaha sana!
Sante ndugu kwa ufafanuzi...simuhukumu yeyote kati yao...[/B]usiseme unashindwa kumtetea yupi, ni sahihi kabisa kuto mtetea yoyote, maelezo yako ni sahii,wote wawili wameitika vibaya katika kutatua matatizo yao. sisi hapa tujifunze tu kutokana na makosa yao na tuache sheria iwahukumu.
pole mume wa nasra kwa kudhalilishwa, pole nasra kwa kuuumizwa na mume, pendaneni sameheaneni
Sasa mbona kakimbia kama sheria inajua?...Kama story hii ni ya kweli, nampongeza huyo mwanaume kwa kumtia adabu. Hata sheria inajua uchokozi si mzuri
Wiki iliyopita tuliongea katika leo tena juu ya kisa cha Marehemu Nasra pichani.Mama huyu alikuwa mkazi wa Bunda mkoani Mara lakini Dar es salaam alifika kufanya matibabu katika hospital ya Muimbili.Kwa miaka takribani 23 alikuwa mke wa bwana Elia Makumbati na kujaaliwa kupata watoto wanne mkubwa kabisa yupo chuo kikuu cha UDOM.Kwa miaka yote wamekuwa na misuko suko sana kwenye ndoa mama akiwa anapigwa sana hata kuchanwa na viwembe.
Mwezi wa pili walitofautiana baada ya bwana kuoa mke mwingine.Wakiwa wametofautiana na Nasra kuendelea na maisha siku hiyo bwana akamfata akamkuta barabarani anatoka kazini.Akiwa na rafiki yake wanatembea akamfungia breki mguuni akamwambia anataka kuongea nae.Nasra akakataa akamwambia kama kuna maongezi hawezi kuongea nae kama vipi amfate nyumbani huku anaendelea kutembea.Bwana yule akamfata kwa nyuma akamgonga na gari na baada ya Nasra kuanguka akanasa chini hivyo kuendelea kumburuza umali wa kama mita 150 hivi.Alipofika kwenye tuta akanasuka bwana ndio kushuka kwenye gari kukimbia.
Kiukweli aliumia sana sana ngozi yote ya mgongoni,mbavuni,makalio,ikavuka na kubaki kwenye lami.Sikio lake la kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7 zilivunjika pamoja na mguu.Akapelekwa hospitali na baadae kulazwa Bugando Mwanza lakini ikawa anahitajika kuhamishiwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.Akiwa muhimbili alikuwa na hali mbaya sana baadae ikathibitika kuwa ameumia ndani kwa ndani kwani alibadilika sana akavimba na kuwa mweusi.Kwamuda wote wa miezi takribani sita alikuwa katika maumivu makali na bahati mbaya hakuweza kupambana tena kupigania maisha yake.